ZURICH, Uswisi
WATU  20 wamefariki dunia baada ya ndege iliyotengenezwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia, kuanguka katika eneo lenye milima Mashariki mwa Uswisi.
Ndege hiyo   ya Junkers JU-52 HB-HOT – ilikuwa na abiria 17 na wahudumua watatu ilipoanza safari yake juzi mchana.
Mmiliki wa ndege hiyo, Shirika la  JU-Air lilisema jana kwamba limehuzunishwa na taarifa hizo na limefuta safari zake zote hadi muda usiojulikana.
Polisi wanasema abiria waliofariki dunia  walikuwa na umri wa kati ya miaka 42 na 84 na kwamba familia zote za waathirika zimejulishwa.
Shirika hilo la JU-Air  huwa linaendesha safari za  utalii kwa kutumia ndege zilizotengenezwa   Ujerumani.
Katika ajali nyingine   Jumamosi iliyopits, watu wanne wa familia moja wakiwamo watoto wadogo walikufa   ndege ndogo ilipoanguka katikati mwa Uswisi.