30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, August 9, 2022

Ndege wa porini watajwa chanzo cha utalii

SEIF TAKAZA – IRAMBA

AINA tofauti 177 za ndege wa porini  wanaopatikana katika tope la Bonde la Wembere katika wilaya nne nchini wanaweza kuwa chanzo kikubwa cha utalii.

Hayo yalisemwa juzi na Ofisa Mali Asili wa Mkoa wa Singida, Charles Kidua wakati alipokuwa akihamasisha uanzishwaji wa  mashamba ya miti ya migunga inayozalisha gundi katika vijiji 14 vya Wilaya ya Iramba mkoani humo.

Kidua alizitaja wilaya hizo kuwa ni pamoja na Ikungi, Kishapu, Igunga na Iramba.

“Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na uhifadhi wa ndege wa porini alisema Mbuga ya tope la Wembere ni makao mazuri ya ndege 177 wa aina tofauti.

Hata hivyo Shirika hilo limetahadhalisha kuwa aina nne za ndege wamo hatarini kutoweka katika mbuga hiyo kwa sababu ya uharibifu mkubwa wa mazingira hivyo miti ya migunga itakayopandwa katika bonde hilo itarejesha mandhari ya mbuga hiyo.

Kidua alisema endapo watalii watakuja kuwaona ndege hao wazuri itasaidia vijana waliopo katika vijiji vilivyopo katika mradi wa mashamba ya migunga kupata ajira.

“Halikadhalika katika mbuga hii ya Wembere kuna vipepeo wazuri, hivyo wajasiriamali  wanaweza wakafanya biashara ya vipepeo kama wanavyofanya sehemu nyingine nchini ambapo wamekuwa kivutio kikubwa katika sherehe mbalimbali’’ alisisitiza Kidua.

Alisisistiza dhamira ya Wakala ya Huduma za Misitu kuanzisha mashamba ya gundi kuwa na shamba pekee nchini mbalo litatoa ajira kwa jamii katika vijiji husika kwa kuwaongezea wananchi chanzo kingine cha mapato.

Meneja wa Wakala wa Misitu Tanzania, Shabani Nyamasagara alisema wazalishaji wakubwa wa gundi ni nchi za Sudan ambayo hutoa tani 50,000 kwa mwaka ,Ethiopia tani 28,000, Nigeria tani 17,000 na Tanzania tani 1,000 kwa mwaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,291FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles