25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Ndege iliyoua abiria 189 yabainika ilikuwa na matatizo

JAKARTA, INDONESIA



NDEGE ya Shirika la Ndege la Lion Air iliyoanguka wiki iliyopita nchini Indonesia na kuua abiria wote 189, iliruhusiwa kusafiri pamoja na kubainika kuwa na matatizo ya kasi angani katika safari zake nne za mwisho.

Wachunguzi wamesema taarifa hizo ni kwa mujibu wa kisanduku cheusi cha kurekodi data za safari cha ndege hiyo, ambayo ni karibu mpya na toleo jipya la Boeing Max 8.

Wakichunguza maudhui ya data, Mchunguzi Mkuu wa Kamati ya Taifa ya Usalama wa Usafirishaji ya Indonesia, ambayo inaongoza uchunguzi wa ajali hiyo, Kapteni Nurcahyo Utomo, alisema; “Tunadhani suala hilio ni muhimu kwa sababu kuna zaidi ya ndege 200 za Max duniani.”

Wakati hakuna ishara kuwa Max 8 ina tatizo la kimfumo katika usomaji wa kasi yake angani, upya wa ndege hiyo unamaanisha uwezekano wa uwepo wa tatizo lolote unaweza kuwa bado haujajitokeza katika ndege za mashirika mengine.

Hata hivyo wataalamu wa anga wameonya ni mapema kuhitimisha chanzo kamili cha ajali hiyo na kwamba taarifa za kisanduku cheusi bado zinahitaji kupitiwa kikamilifu.

Aidha timu za waokozi zinaendelea kutafuta kisanduku kingine cha kurekodi data za safari.

Ndege hiyo ya Lion Air aina ya JT610 ilianguka katika bahari ya Java dakika 13 baada ya kupaa kutoka mji mkuu wa Indonesia wa Jakarta.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles