Ndege iliyobeba abiria 188 yaanguka Indonesia

Jakarta, Indonesia


Ndege ya shirika la Lion Air Boeing 737 iliyokuwa ikisafiri kutoka mji Mkuu wa Indonesia kwenda Pangakal Pinang imeanguka muda mfupi baada ya kuruka angani katika uwanja wa ndege wa Jakarta.

Taarifa iliyotolewa na maafisa wa Indonesia imesema kuwa Ndege yenye namba za usajili JT-610 ilikuwa imebeba abiria 188 ambapo 178 watu wazima, watoto watatu, Rubani wawili pamoja na wahudumu wa tano.

Wakati huo huo, Msemaji wa Shirika la  huduma za uokoaji nchini humo, Yusuf Latif,  amethibitisha kwa waandishi wa habari kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa bado jitihada za kujua chanzo cha ajali ya ndege hiyo zinaendelea.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here