26.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Ndayiragije: Tutawapiga Harambee Stars kwao

Theresia Gasper -Dar es salaam

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Etienne Ndayiragije, amesema bado wana nafasi ya kuwafunga Kenya katika mchezo wa marudiano wa kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan).

Taifa Stars, juzi ilishindwa kutamba nyumbani baada ya kulazimisha suluhu Harambee Stars, ukiwa ni mchezo wa kwanza baina ya timu hizo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Timu hizo zinatarajia kurudiana Agosti 4, mwaka huu, nchini Kenya.

Akizungumza Dar es Salaam juzi baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Ndayiragije, alisema mchezo wa kwanza ulikuwa na presha ukizingatia walikuwa nyumbani hali iliyowafanya wacheze kwa tahadhari kubwa.

“Tumetoka suluhu nyumbani, matokeo ambayo sio mazuri kwa upande wetu, lakini kupitia mechi hii, tumeweza kuwafahamu vizuri wapinzani wetu, hivyo naamini tutapata matokeo kwenye mchezo wa marudiano,” alisema.

Alisema licha ya matokeo hayo, wachezaji wake waliweza kupambana na kukosa mabao mengi, hivyo atayafanyia kazi tatizo hilo kuelekea mchezo wa marudiano.

Ndayiragije alisema licha ya mchezo wa ugenini kuwa mgumu, lolote linaweza kutokea kwani hata wapinzani wao wameweza kulazimisha sare ugenini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,206FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles