Ndayiragije: Hakuna aliye salama kudumu Stars

0
745

THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KAIMU Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania, Taifa Stars, Etienne Ndayiragije, amesema hakuna mchezaji mwenye namba ya kudumu katika kikosi hicho kwani kila mara kinabadilika.

Ndayiragije aliyerithi mikoba ya Mnigeria Emmanuel Amunike, ameisaida Taifa Stars kutinga hatua ya pili ya michuano ya kufuzu Kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan 2020), baada ya kuitoa Kenya kwa ushindi wa jumla wa penalti 4-1.

Mbali ya hilo, kocha huyo pia ameiwezesha Stars kutinga hatua ya makundi ya kuwania tiketi ya fainali za Kombe la Dunia 2022, nchini Qatar, ikiitoa Burundi kwa mikwaju ya penalti 3-0, baada ya sare ya bao 1-1 katika mechi zote mbili za nyumbani na ugenini.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Ndayiragije alisema hawezi kusema Juma Kaseja atakuwa kipa namba moja wa kudumu katika kikosi hicho kwani anaweza akaitwa yeyote.

“Mchezaji yeyote anaweza akaitwa timu ya Taifa, kwa sababu kikosi hiki kinaweza kikabadilika kutokana na uwezo atakaoonyesha mchezaji kwenye timu yake,” alisema.

Alisema hadi sasa hakuna timu ya Taifa hadi hapo atakapotaja tena kikosi kwa ajili ya mchezo wao wa Chan dhidi ya Sudan.

Kocha huyo muda wowote kuanzia sasa anaweza kutangaza kikosi cha Stars kitakachoingia kambini hivi karibuni kujiandaa na mchezo huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here