24.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

Ndalichako atoa rati za ya mitihani ya taifa

Mwanandishi Wetu, Dar es Salaam

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako ametangaza ratiba za mitihani ya taifa darasa la saba, kidato cha nne na upimaji wa kitaifa wa darasa la nne na kidato cha pili.


Pro. Ndalichako ametangaza ratiba hiyo leo Jumatano Juni 17, baada ya Rais John Magufuli kuagiza shule zote za msingi na sekondari kufunguliwa Jumatatu Juni 29, ikiwa ni pamoja na kuruhusu shughuli nyingine za kijamii zilizokuwa zimezuiwa kuendelea kama kawaida.


“Wizara ya Elimu imepokea maagizo ya Rais Magufuli kwa furaha na tuko tayari kusimamia wanafunzi kuendelea na masomo hivyo ninapenda kutoa taarifa kuhusu mihula mipya ya shule na ratiba za upimaji wa kitaifa wa darasa lanne na kidato cha pili, mtihani wa kumaliza elimu ya msingi na kidato cha nne,” amesema Pro. Ndalichako.


Amesema kwa shule za msingi na sekondari wanafunzi watareje shuleni Juni 29, mwaka huu na kumaliza muhula wakwanza wa masomo Agosti 28, mwaka huu na kuanza muhula wa pili ambao utaisha Desemba 18, mwaka huu.
“Ili kukamilisha muhtasari wa masomo shule zitalazimika kuongeza saa mbili za masomo ili kufidia muda uliopotea, maelekezo ya kuongeza muda hayatahusisha madarasa ya awali.


“Kwa wanafunzi wa kidato cha tano wataripoti shuleni Juni 29, mwaka huu kama ilivyotangazwa, watasoma na kukamilisha muhtasari wa kidato cha tano Julai 24 na wanafunzi hawa wataanza rasmi masomo ya kidato cha sita Julai 27, mwaka huu,” amesema Pro. Ndalichako.


Ratiba ya mitihani ya darasa la saba (PSLE) itaanza Oktoba 07 hadi Oktoba 08 mwaka huu, Kidato cha pili (FTNA) kuanzia Novemba 09 hadi Novemba 20 mwaka huu, Kidato cha nne (CSEE) kuanzia Novemba 23 hadi Desemba 11 mwaka huu na Darasa la nne (SFNA) kuanzia Oktoba 25 hadi Oktoba 26 mwaka huu.


Aidha Pro. Ndalichako amesisitiza uongozi wa shule zote nchini kuhakikisha wanafunzi, walimu na wafanyakazi wote wanazingatia maelekezo ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona kama yalivyotolewa na Wizara ya Afya na kuhakikisha kuwa shule zinanunua vifaa vya kutosha kwa ajili ya kunawa mikono kwa maji yanayotoririka na sababu.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

12,054FansLike
2,941FollowersFollow
18,400SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Latest Articles