24.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Ndalichako aridhishwa na ukarabati shule aliyosoma Nyerere

Mwandishi wetu

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako, amekagua maendeleo ya ukarabati na upanuzi wa shule ya msingi  Mwisenge na kuridhishwa na kasi na ubora wa kazi inayoendelea.

Ukarabati wa Shule ya hiyo ambayo alisoma baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ulianza kufanyika baada ya Rais wa John Magufuli kuitembelea na kuagiza ikarabatiwe na kujengewa ukuta ambapo hivi sasa umefikia asilimia 60.

Akizungumza katika ziara ya kukagua maendeleo mradi huo Ndalichako amesema ameridhishwa na kasi hiyo ya ujenzi huo ambao unahusisha ukarabati wa majengo ya kale, ukarabati wa madarasa, mabweni, ujenzi wa madarasa na mabweni mapya, ujenzi wa uzio kuzunguka shule hiyo, ukarabati wa mnara wa kumbukumbu pamoja na uboreshajii wa mazingira ya nje.

“Nimefurahishwa na hatua iliyofikiwa mpaka sasa na viwango vya ujenzi wa madarasa na mabweni nao ni imara, hata ujenzi wa ukuta unafanyika vizuri, kuta za mabweni ni ndefu na zitawafanya watoto wakiwa ndani wapate hewa vizuri” amesema.

Shule hiyo awali ilikuwa haina ukuta kabisa hali ambayo ilisababisha mazingira kuwa hatarishi kwa watoto hasa wenye ulemavu wa Ngozi.

Mradi huo unaogharimu sh milioni 706 ambazo zimetolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ulianza Mwezi April na utakamilika na kukabidhiwa mwezi Septemba mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,211FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles