22.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Ndalichako akabidhi magari 39 kwa vyuo vya ualimu

Tunu Nassor-Dar es Salaam

Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia imekabidhi magari 39 kwa vyuo vya ualimu vya serikali nchini ili kurahisisha utendaji kazi wake.

Akikabidhi msaada uliotolewa na mashirika wa maendeleo ya elimu jijini Dar es Salaam huo leo Jumatatu Januari 13, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema magari hayo yalete matokeo chanya na kazi ifanyike kwa wepesi.

Amesema fedha zinazotolewa na wafadhili zitaendelea kusimamiwa vema ili zifanye kazi iliyokusudiwa na kuahidi kuongeza uwekezaji katika sekta ya elimu.

Profesa ameonya matumizi mabaya ya magari hayo ikiwamo kubeba mizigo isiyostahili (isiyosema), bali yatumike kwa lengo liliyokusudiwa.

“Msiende kuyaua haya magari mkayape huduma zote kwa wakati mkishindwa kuyatunza na sisi tutakula sambamba na ninyi.”amesema Profesa Ndalichako.

Amesema magari mengi ya vyuo yapo juu ya mawe jambo ambalo linafanya ugumu wa utendaji kazi ndani ya vyuo hivyo.

“ Chuo kimoja kina wanafunzi zaidi ya 1000 hivyo kukosekana kwa magari ni shida …tunaomba haya yaliyopatikana yatumike kama ilivyokusudiwa na sio kubebea mizigo isiyostahili,”amesema Joyce.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,717FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles