28.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Ndalichako aingilia kati wanafunzi waliofutiwa usajili UDSM

Asha Bani, Dar es SalaamWaziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, ameagiza wanafunzi 682 walioondolewa katika usajili wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam kurudishwa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Oktoba 22, muda mfupi baada kufungua mafunzo ya wahasibu yanayoendelea jijini Dar es Salaam Profesa Ndalichako amesema amesikia suala hilo mwishoni mwa wiki na tayari ameshauagiza uongozi wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) na uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kukaa pamoja na kumaliza tofauti hizo.

“Chuo Kikuu kina nafasi 3,000 tatizo lilikuwa ni la kiufundi kutokana na wanafunzi wengi kupenda chuo hicho ,hivyo nimeomba uongozi kumaliza tatizo hilo na watoto waweze kupokelewa.

“Wengi wanapenda UDSM na tatizo lilikuwa linaweza kurekebishika na wote ni idara za serikali, TCU na UDSM hawakutakiwa kushindana na ndiyo maana nimewaagiza hadi Jumamosi wawe wamemaliza tofauti zao nafikiri hadi leo saa tisa watakuwa wameshawekana sawa,” amesema Profesa Ndalichako.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles