27.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

Ndalichako ahimiza ubunifu kuelekea Tanzania ya Viwanda

Anna Potinus

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Joyce Ndalichako amewaagiza wanafunzi wanaosoma masomo ya Sayansi na wabunifu nchini kubuni vitu ambavyo vitasaidia kurahisisha shughuli mbalimbali.

Amesema hayo leo Alhamisi Machi 7, katika kilele cha Mashindano ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu  (MAKISATU) jijini Dodoma ambayo kauli mbiu yake ni ‘kukuza ujuzi na ubunifu kwa uchumi wa viwanda’ ambapo amesisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kuonyesha ubunifu wao ili kukuza uchumi wa nchi.

“Changamoto tuliyonayo kwa sasa ni muamko kwa wananchi haujafikia katika kiwango ambacho serikali ingependa kukiona, ni wazi kabisa tunapaswa kuwa na ubunifu na kutumia sayansi na teknolojia kuhakikisha tunarahisisha maisha ya wananchi wanaoishi vijijini.

“Ninatoa wito kwa wabunifu wote nchini kuhakikisha wanajikita kuangalia ni kwa namna gani wanarahisisha shughuli zinazofanyika katika mazingira yao na ikumbukwe ubunifu hauna umri na hauchagui kwasababu mwisho wa siku mkono unaenda kinywani,” amesema.

Aidha Ndalichako amesema washindi waliopatikana katika mashindano hayo wataendelezwa ili waweze kukuza tafiti zao kwa lengo la kukuza uchumi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,903FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles