22.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Nchi za Kiarabu zaupinga uamuzi wa Trump

TUNIS, TUNISIA

VIONGOZI wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu katika mkutano wao wa kilele uliofanyika mjini hapa juzi

wameupinga kwa kauli moja uamuzi wa Marekani wa kuitambua milima ya Golan kama sehemu ya Israeli.

Katika tamko la mwisho baada ya mkutano wao wa kilele kumalizika, viongozi hao walisema wanasisitiza kuwa milima hiyo inayokaliwa na Israel ni eneo la Syria, kwa mujibu wa sheria ya kimataifa, maamuzi ya Umoja wa Mataifa na ya Baraza la Usalama.

Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo, Ahmed Aboul Gheit amesema hoja ya Rais Trump ni batili, si halalikabisa.

Wiki iliyopita, Rais Trump alitia saini tamko la kuitambua milima ya Golankuwa sehemu ya Israel.

Israel iliiteka milima hiyo wakati wa vita vya mwaka 1967 vya mashariki ya kati baada ya Syria kuitumia sehemu hiyo umuhimu wa kijeshi, kwa ajili ya kushambulia sehemu za kaskazini mwa Israel. Israel ililiunganisha eneo hilo katika milki yake mwaka 1981.

Kwa muda wa miaka mingi nchi za Kiarabu zimekuwa zinataka eneo hilo lirudishwe Syria na hivyo uamuzi wa Trump kuitambua milima hiyo kuwa ni sehemu ya ardhi ya Israel umewakera.

Viongozi wa Kiarabu wamesema watawasilisha azimio kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupinga uamuzi wa Marekani na pia wameahidi kuwaunga mkono Wapalestina katika jitihada zao za kutaka uhuru wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,415FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles