24.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 8, 2022

Nchi tisa kushiriki uchunguzi usalama wa Boeing 737 MAX

NEW YORK, Marekani

MAMLAKA ya Usalama wa Anga nchini hapa (FAA), imesema kwa kushirikiana na serikali, itaanza kuzipitia tena upya ndege aina ya Boeing 737 MAX, zilizosimamishwa kufanya kazi kuanzia Aprili 29 mwaka huu na watashirikiana na mamlaka nyingine kutoka mataifa tisa.

Taarifa hiyo imetolewa baada ya mapema mwezi huu, FAA kutangaza kwamba imeunda timu ya kuchunguza hali ya usalama wa ndege hizo ambazo zimesimamishwa kufanya kazi katika maeneo mbalimbali duniani kufuatia ajali mbili zilizotokea mwezi uliopita Indonesia na Ethiopia na kusababisha vifo vya watu 350.

Kampuni ya Boeing ilitangaza kuifanyia marekebisho programu iliyopo katika ndege hizo aina ya 737 MAX ambayo inachunguzwa kufuatia ajali hizo mbili.

Hata hivyo mpaka sasa haijawasilisha programu hiyo kwa FAA na sasa mamlaka za anga za China, Ulaya, Canada, Brazil, Australia, Japan, Indonesia, Falme za Kiarabu, (UAE) na Singapore zitashiriki katika kazi hiyo ambayo inatarajia kuchukua miezi mitatu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,235FollowersFollow
549,000SubscribersSubscribe

Latest Articles