31 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

Nchi gizani kwa saa 12 wiki nzima

tanekoNA SHABANI MATUTU, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limetangaza kuanza kukata umeme leo kwa mikoa inayotumia gridi ya taifa kwa   wiki moja kwa  saa 12 kila siku.

Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco,   Felchesmi Mramba alitaja baadhi ya mikoa ambayo itakumbwa na tatizo hiyo kuwa ni   Dar es Salaam, Mbeya,  Lindi, Mwara, Mwanza, Arusha na mingine.

Alikuwa  akizungumza na wandishi wa habari  jana kwenye ziara   ya kutembelea mitambo ya Kinyerezi na Ubungo,  Dar es Salaam.

“Umeme utazimwa kila siku kwa   wiki moja kwa saa 12,  kuwezesha mitambo ya Symbion na Ubungo 2 ipate kuunganishwa kwenye gridi ya taifa kwa kutumia nishati ya gesi,” alisema.

Mramba alisema wakati   mitambo hiyo inayotumia gesi itakapozimwa, mtambo pekee utakaobaki ukifanyakazi ni  Ubungo 1 ambao unaendesha mikoa michache ambayo haiko kwenye gridi ya Taifa.

Alisema kazi ya kuunganisha mitambo hiyo inatarajiwa kukamilika katika wiki moja na itawezesha kukamilika  mradi huo uliozinduliwa miaka miwili iliyopita na Rais Jakaya Kikwete.

Mramba alisema kama mradi huo utafanikiwa, mitambo ya Symbion pekee itazalisha umeme wa Megawatt 102, mtambo    wa Ubungo 2 utazalisha Megawatt 105.

Akielezea faida zitakazopatikana baada ya kukamilika  mtambo huo Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk. James Mataragio alisema ni pamoja na Watanzania kupata umeme wa uhakika.

Faida nyingine ni kuondokana na utegemezi wa kuzalisha umeme kwa kutumia mafuta yaliyokuwa yakiipa Tanesco hasara ya Sh  bilioni moja kwa mwaka.

Dk. Mataragio alisema hatua hiyo pia itasaidia kutunza mazingira kwa kutumia gesi ikilinganishwa na aina nyingine ya nishati inazotumiwa likiwamo na ongezeko la shughuli za uchumi kwa watu wa kawaida kutokana na ajira mpya.

Mkurugenzi huyo alitaja faida nyingine kuwa ni kuanza  uzalishaji wa umeme kwenye mashine zilizopo Ubungo zenye uwezo wa Megawatt 200 ambazo zilikuwa hazipati gesi ya kutosha.

Dk. Mataragio alisema uzalishaji huo utasaidia kuongezeka shughuli za utafiti na uendeshaji wa mafuta na gesi nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles