24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Nchi 11 Afrika kusaidiwa vita ya corona

 MWAANDISHI WETU– DAR ES SALAAM 

KAMPUNI ya ukopeshaji ya Letshego Holdings Ltd, imetenga Sh milioni 580 kusaidia nchi 11 zilizopo kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika, kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya corona.

Fedha hizo zitaelekezwa moja kwa moja katika akaunti ya mfuko wa taifa wa kila nchi, zikiwa na lengo la kuutokomeza ugonjwa ambao kwa sasa unaendelea kuua watu wengi duniani.

Mtendaji Mkuu wa Letshego Tanzania Limited (Faidika), Baraka Munisi alisema pamoja na kampuni yao kushughulika na masuala ya ukopeshaji fedha, wameamua kuunga mkono kupiga vita maambukizi ya ugonjwa wa corona ambao umeathiri shughuli mbalimbali uchumi.

Alisema Tanzania imepokea msaada wa vifaa vyenye thamani ya Sh milioni 33 kwa ajili ya kupambana na virusi vya corona, ambao ilikabidhiwa kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Alisema wamechukua hatua kubwa ya kuwasaidia wateja wake kutokana na changamoto zinazoendelea kutokea zilizosababishwa wa virusi vya corona.

“Letshego imetoa malipo ya ahueni kwa wajasiriamali wote wadogo na wa kati na vile vile kutoa fursa kwa wateja wote kuomba kulipa mikopo kwa unafuu kutokana na kupungua kwa shughuli za kiuchumi katika masoko ya kanda yote. 

Alisema ili kukabiliana na maambuziki ya virusi vya ugonjwa huo,wameamua kupunguza wafanyakazi wake wa masoko, badala yake imebaki nao wachache ili kuhamasisha mwongozo wa wataalam wa afya.

Alisema kampuni yao, pia itahamasisha wateja wake kutumia mitandao yao ya kidigitali ili kupata taarifa za akaunti pamoja na kufanya maombi ya mkopo. 

“Afya na ustawi wa wafanyakazi na wateja wetu inabaki kuwa kipaumbele chetu. 

Tunawasaidia wateja jinsi ya kutumia teknolojia na uendeshaji kwa kutumia miundombinu yetu salama ya kidijiti. 

Wateja wanahamasishwa kutumia mitandao ya kidijiti kama vile barua pepe, WhatsApp na kupiga simu kupitia huduma kwa wateja ambayo tumeongeza muda wa huduma kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa mbili usiku,” alisema.

Alisisema itaendelea kushirikiana na Serikali na mamlaka za afya kuhamasisha miongozo rasmi ya afya, pia kuungana na ushauri wa kimataifa wa afya kutoka Shirika la Afya Duniani(WHO) na kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles