Na Ramadhan Hassan, Mtanzania Digital
Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) limejipanga kukamilisha muongozo wa gharama za ujenzi wa barabara nchini kwa kuandaa gharama za msingi za mkandarasi katika kutekeleza kazi mbalimbali za ujenzi wa barabara kwa kila Mkoa Tanzania Bara.
Hayo yameeelezwa Februari 13,2023 jijini Dodoma na Mtendaji Mkuu wa baraza hilo, Dk Samson Mturi wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya baraza hilo kwa waandishi wa habari.
Amesema lengo la kukamilisha muongozo huo ni kuhakikisha mambo yanakaa sawa katika sekta ya ujenzi.
Pia amesema wamepanga kuandaa mapendekezo ya kuboresha sheria na miongozo inayosimamia ujenzi wa majengo nchini.
“Kusimamia utatuzi wa migogoro itakayotokea katika miradi ya ujenzi pamoja na kutoa ushauri wa kifundi kwa wadau mbalimbali wa sekta ya ujenzi,”amesema Mtendaji huyo.
Amesema mwelekeo wa Baraza hilo ni kufuatilia sera ya ujenzi pamoja na kuandaa na kutekeleza Mpango mkakati wa Maendeleo ya sekta ya ujenzi.
“Kutoa miongozo mbalimbali ya kitaaluma ya maeneo mbali ya ujenzi,”amesema Mkurugenzi huyo.