26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

NBTS waja na kampeni ya kutokomeza vifo vitokanavyo na uzazi

AVELINE KITOMARY

Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS), umeandaa kampeni ya siku tano wenye lengo la kutokomeza vifo vitokanavyo na uzazi vinavyosababishwa na ukosefu wa damu.

Akizungumza na MTANZANIA katika Mahojia maalum Mkuu wa Idara ya Ukusanyaji damu, Dk. Aveline Ngasa amesema wanatarajia kukusanya chupa 32,700 za damu nchi nzima.

Dk. Aveline amesema ukusanyaji damu huo unaambatana na kampeni iliyoanza jana Septemba 21 hadi 25 kwa kulenga maeneo yote ya mijini na vijijini na kwamba katika kampeni hizo kauli mbiu ni ‘Damu salama Uhai wa mama’.

“Ukosefu wa damu unasababisha vifo vya kinamama ambapo moja ya tatu ya vifo hutokea kwasababu hiyo  na ripoti ya Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia ,Wazee na Watoto  ya mwaka 2015/16 inaonesha kuwa kuna vifo 556 kwa kila kizazi 100,000 na vifo hivyo ni asilimia 18  ya vifo vyote vya wanawake  wenye umri  chini ya miaka 15-49.

“Mama napoenda kujifungua katika kituo cha afya anaweza kupata shida ya kuvuja damu na akahitaji kuongezewa lakini kama  haipo ataongezwa nini? Hii husababisha kupoteza maisha,”amesema Dk Aveline.

Amesema kuwa wanaendelea kutoa elimu kwa jamii ili waweze kujitokeza kuchangia damu na kufikia lengo la ukusanyaji damu katika kampeni hizo.

“Hadi sasa kiasi cha mwitikio sio kidogo watu wanajitokeza kuchangia damu lakini tunataka kufikia matarajio yetu hivyo tutaendelea kuhamasisha watu wajitokezwa zaidi.

“Kila mwaka uhitaji wa damu ni chupa 550,000   hii ni sawa na asilimia  moja ya idadi ya watanzania  na tumejigawa kwa timu ya Halmashauri 185  wanatakiwa kukusanya chupa 150 kwa kila mmoja,hospitali za kanda  chupa 500,timu ya mikoa  chupa 150  na timu ya damu salama  vituo vya kanda chupa 500,”amesema Dk Aveline. 

Dk Aveline alitoa wito kwa jamii kuendelea kujitokeza kuchangia damu kwa hiari ili kuweza kufanikisha kampeni hizo.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles