25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

NBS: TAKWIMU ZA KUPIKA ZIMEPUNGUA

 

Mwandishi Wetu, Morogoro       |


Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), imesema tangu Sheria ya Takwimu Namba 9 ya mwaka 2015, ilipoanza kazi hali ya upotoshaji wa takwimu nchini imepungua.

Akizungumza leo Jumamosi Juni 9, mjini Morogoro, Mwanasheria wa NBS, Oscar Mangula, amesema pamoja na kupungua kwa hali hiyo bado vyombo vya habari vina wajibu wa kutoa elimu sahihi kwa umma kuhusu sheria hiyo.

“Kwa sasa matukio ya takwimu za kupika yamepungua tofauti na awali ambapo watu walikuwa wakipika takwimu kinyume cha sheria.

“Hata hivyo bado sheria hii ya mwaka 2015, NBS ndiyo ina wajibu wa kusimamia suala hili. Na tunawaomba Watanzania watoe ushirikiano na pindi wanapohitaji ufafanuzi milango yetu ipo wazi, ” amesema Mangula

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles