31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

NBS: MFUMUKO WA BEI UMESHUKA

LEONARD MANG’OHA – dar es salaam                                                       OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS), imetangaza kushuka kwa mfumuko wa bei ya bidhaa kutoka asilimia 5.4 Juni mwaka huu hadi 5.2 mwezi uliopita.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo, alisema hali hiyo inatokana na kupungua kwa bei za bidhaa za huduma na vyakula kwa kipindi kilichoishia Julai, mwaka huu.

“Baadhi ya bidhaa za vyakula vilivyochangia kupungua kwa mfumuko wa bei, ni pamoja na nyama asilimia 3.8, samaki wabichi asilimia 14.1, dagaa asilimia 8.4, kabichi asilimia 16.6, bilinganya asilimia 10.6, vitunguu asilimia 13.2, karoti asilimia 16.9, njegere asilimia 15.7 na viazi mviringo asilimia 13.5,” alisema Kwesigabo.

Alisema mfumuko wa bidhaa za vyakula nyumbani na migahawani kwa mwezi Julai umepungua hadi asilimia 9.3 kutoka asilimia 9.8 ya mwezi Juni,” aliongeza.

Kwesigabo alisema fahirisi za bei zimeongezeka hadi 108.85 Julai 2017,kutoka 103.50 Julai mwaka jana.

Alisema pia thamani ya shilingi ya Tanzania imezidi kuimarika na sasa uwezo wa Sh 100 katika kununua bidhaa na huduma umefikia Sh 91.87 kwa mwezi Julai, mwaka huu ikilinganishwa na Sh 91.66 ilivyokuwa Juni.

Pamoja na hali hiyo, mfumuko huo umeonekana kuwa na mwelekeo unaofanana na baadhi ya nchi nyingine za Afrika Mashariki.

“Nchini Kenya, mfumuko wa bei wa mwezi Julai umepungua hadi asilimia 7.47 kutoka asilimia 9.21 kwa mwezi Juni, huku nchini Uganda umepungua hadi asilimia 5.70 kwa mwezi Julai kutoka asilimia 6.4 mwezi Juni,” alisema Kwesigabo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles