23.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 22, 2023

Contact us: [email protected]

NBC yafungua akaunti ya malengo kwa wananchi

Ferdnanda Mbamila, Dar es Salaam

Benki ya NBC imefungua akaunti ya malengo, inayojulikana kama Ibuka kidedea kwa malengo akaunti.

Akaunti hiyo imezinduliwa leo Jumatatu Septemba 30, kwa ajili ya wateja na wananchi kwa ujumla.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya ufunguzi huo katika tawi la NBC DUCE jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa huduma kwa wateja, Doroth Magonye amesema akaunti hiyo ni ya kuhifadhi fedha kwa  wafanyabiashara wote na wananchi.

Amesema kampeni ya hiyo ya malengo itadumu kwa muda wa miezi 6 ambapo mshindi atakeyepatikana atapata zawadi ya pikipiki na tiketi ya kwenda kutalii katika mbuga ya wanyama ya mikumi kwenda kupumzika.

Amesema kuwa hadi sasa kuna pikipiki 20 za miguu miwili, pikipiki 20 za miguu mitatu na kuna tiketi sita kwa yeyote atakayeshinda.

”Akaunti ya malengo ni mahususi kwa ajili ya malengo ya ada, kulipia mashamba, nyumba, pia benki inatoa asilimia saba kwa kila mteja anyetumia,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles