27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Naweza Tanzania, Mwijaku waja na ‘Couple Challenge’

JEREMIA ERNEST

JUKWAA la Naweza Tanzania na muigizaji Burton Mwambe ‘Mwijaku,’ wameanzisha kampeni inayolenga kukuza ustawi wa afya katika familia ili kuweza kuishi kwa furaha na upendo.

Akizungumza na waandishi wa habari balozi wa kampeni hiyo Mwijaku, amesema wamezindua rasmi ‘Naweza Couple Challenge’ ambapo kwa kupitia familia nane watu watapata fursa ya kujifunza ni jinsi gani wameweza kudumisha upendo na furaha katika familia zao.

“Nitaendesha zoezi hili kwa miezi mitatu nikishirikiana na Smart Generation, ili kupata couple moja itakayoshinda katika shindano hili lenye lengo la kudumisha amni katika jamii,” alisema Mwijaku.

Aliongeza kuwa zawadi za washindi zitatolewa kupitia ukurasa wa wake katika mitandano ya kijamii, kupitia shindano hilo litachangia kukuza kizazi makini chenye afya bora.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles