30 C
Dar es Salaam
Friday, January 27, 2023

Contact us: [email protected]

NATAMANI KUONA WASANII WETU WAKITAJIRIKA

MCHANGO wa wasanii ni mkubwa sana katika jamii yetu. Kupitia kazi zao za fasihi jamii imeweza kuelimika, kuburudika na mengine mengi.

Lakini pia wasanii wamekuwa chachu katika kufikisha ujumbe kupitia sanaa kwenye mambo mbambali kwa jamii yetu. Kwa hakika hatuwezi kuwabeza wasanii wetu maana wana mchango mkubwa sana.

Tangu enzi, wasanii wamekuwa wakishiriki kwenye kampeni za kuhamasisha jamii mfano majanga au hafla. Tunakumbuka namna wanamuziki wa zamani walivyokuwa wakiimba nyimbo za shughuli mbalimbali kama Sabasaba (sasa Nanenane) na nyinginezo.

Lakini pamoja na hayo, wasanii wetu wamekuwa katika mazingira magumu ya kupata stahiki zao kupitia kazi zao. Mara kadhaa wamekuwa wakilalamika kuhusu kuibiwa kazi zao za kiubunifu lakini kulazimika kuingia katika mikataba mibovu inayozingatia masilahi ya wenye nazo pekee na kuwaacha wasanii hohehahe.

Hivi karibuni wasanii wawili wakubwa wa Bongo Fleva walilalamikia kazi zao kutumika bila ridhaa yao na kupewa haki zao, lakini hata wale wa filamu nao wamekuwa wakilalamika namna wanavyolipwa kidogo huku wakiwa hawana pa kukimbilia.

Serikali ina uwezo wa kutatua na kulinda haki za wasanii wetu. Natamani kuona siku moja wasanii wetu wakiishi maisha mazuri kulingana  na ukubwa wa juhudi zao.

Rais Mstaafu, Dk. Jakaya Kikwete alianza vizuri kazi ya kuiweka serikali na wasanii wetu karibu. Lakini inatia faraja zaidi baada ya Rais Dk. John Magufuli kuamua kuwaunganisha wasanii katika iliyokuwa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (ya serikali ya awamu iliyopita hadi kuwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo chini ya Waziri Nape Nnauye.

Natambua nia njema ya Rais wetu kwa wasanii, basi ni vizuri pia kama serikali itatafuta namna ya kusimamia kazi za wasanii wetu ili wanufaike kutokana na kazi zao za ubunifu.

Kwa hakika inawezekana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles