22 C
Dar es Salaam
Sunday, May 28, 2023

Contact us: [email protected]

Nape kufungua Kongamano la 12 la kitaaluma la TEF mjini Morogoro

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye anatarajiwa kufungua Kongamano la 12 la Kitaaluma la Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), linalotarajiwa kuanza Machi 29, 2023, mjini Morogoro ambapo .

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TEF, Neville Meena amewaambia Waandishi wa Habari mapema leo Machi 27, mjini Morogoro kuwa pamoja na Nape, pia jukwaa hilo linategemea kuwepo mgeni mwingine ambaye ni Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Damas Ndumbaro.

“Kongamano hili huwa tunafanya kila mwaka kwenye mikoa mbalimbali, safari hii tumeamua kufanyia hapa Morogoro,” amesema Meena.

Meena amesema katika kongamano hilo, kutakuwa na mada sita ambazo ni Utendaji wa Vyombo vya Habari, Taaluma na Maadili; Wanawake katika habari na hatari ya kutoweka kwao kwenye vyumba vya habari.

Amezitaja mada nyingine kuwa ni Uchumi wa Vyombo vya Habari na jinsi ya kuvinusuru; Mabadiliko ya Teknolojia, Ukuaji na Ujenzi wa Mitandao ya Kijamii yenye viwango vya kitaaluma; Mchakato wa Mabadiliko ya Sheria za Habari na mweleko wake.

Amesema, mada ya mwisho itakuwa Vyombo vya Habari na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu wa 2025.

“Uchaguzi sio tukio, ni mchakato. Inahitajika kuandaa watu na kuwashawishi kushiriki kwenye uchaguzi, vyombo vya habari vinawekeza fedha kwenye uchaguzi huo, hivyo ni sehemu muhimu kwenye kongamano hili,” amesema.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TEF, Jane Mihanji.

Upande wake Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TEF, Jane Mihanji amesema miongoni mwa sababu za kuweka mada inayohusu wanawake na vyombo vya habari ni kutokana na tafiti kuonesha kwamba, kuna unyanyasaji wa wanawake kwenye vyombo vya habari.

“Tumekuwa tukihimiza kuwa na ushiriki sawa. Baadhi ya tafiti zinaonesha wanawake wanaopewa nafasi za juu ni wachache. Tafiti za TAMWA, Internews na zingine zinaonesha kuwa, kumekuwa na unyanyasaji wa wanawake kwenye vyumba vya habari. Taarifa zao zimekuwa hazitoki hivyo, wamekuwa wakikimbia vyumba vya habari,” amesema Mihanji.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Mada zote zilizoandaliwa ni vyema zifanyiwe kazi-“mtulipotie nasi wananchi tuzijue!”- maana zinaguza jamii

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,169FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles