25 C
Dar es Salaam
Sunday, October 6, 2024

Contact us: [email protected]

Nani wa kumtetea Ozil Arsenal?

ADAM MKWEPU NA MITANDAO

Mesut Ozil kuendelea kuwapo katika kikosi cha Arsenal msimu ujao ni kama ndoto.

Safari ya kuondoka viunga vya Londoni ya Kaskazini imewadia kwa kiungo huyo mahiri ambaye ni muhanga wa ujio wa Unai Emery pale Arsenal tangu Arsene Wenger aondoke  baada ya kuiongoza timu hiyo kwa miaka 22.

Tangu Emery atue katika klabu hiyo Juni mwaka jana amemuonyesha kisogo Ozil kwa madai kuwa hana imani kama atamudu mfumo wake na kwa sababu hiyo haoni haja nyota huyo kuendelea kuwapo katika klabu hiyo.

Inter Milan  ambao walikaribia kuinasa saini yake nao wamebadili upepo wameweka wazi kuwa hawamtaki na hawana mpango naye.

Emery anaamini Arsenal inaweza  kushinda mataji bila Ozil hivyo wapo tayari afungashe virago aondoke.Ni uamuzi wake aondoke sasa au baadae lakini kocha amtaki.

Taarifa zinaonyesha kuwa kwa sasa Ozil ameanza kuungwa mkono na mashabiki katika bifu lake na Emery na kama hali itakuwa kama ilivyo huenda akashinda  kwa nguvu za nje ya uwanja.

Mashabiki hawaonyeshi kufurahishwa na kitendo cha Ozil kuwekwa benchi  kwani hata katika mchezo wa Ligi ya Europa dhidi ya BATE  uliochezwa Alhamisi iliyopita ambao Arsenal ilifungwa bao 1-0,  baadhi yao walikuwa na mabango  yaliyokuwa na ujumbe uliotaka Emery atimuliwe.

Lakini Mhispania huyo anadai hawezi kumtumia Ozil katika michezo muhimu inayohitaji ushindi kwa maneno mepesi hana msaada.

Licha ya kikosi cha Emery kuwa imara zaidi eneo la ushambuliaji akiwamo Ozil wakati timu hiyo ilipopata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Leicester City, lakini Emery anasema vijana wake wanaweza kufanya makubwa bila uwepo wa nyota huyo mwenye jezi namba 10.

Katika mchezo dhidi ya West Ham,  Ozil  anadaiwa alifanya mandalizi kabambe wiki mbili kabla ya mchezo lakini mwisho wa siku akajikuta hayupo hata kwenye benchi la wachezaji wa akiba.

Lakini huu unafahamika kama mpango maalumu kwa Emery kulazimisha kiungo huyo aondoke.

Mara ya mwisho kucheza kikosi cha kwanza ilikuwa wiki sita zilizopita katika mchezo dhidi ya Brighton tangu hapo  Ozil ametumika mara mbili kikosi cha Arsenal.

Katika mchezo dhidi ya Brighton nyota huyo aliondolewa  kipindi cha kwanza na ilimlazimu kukaa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja akisubiri apangwe tena  katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Manchester United ambao Arsenal ilifungwa mabao 3-1.

Nyota huyo  alipoanza katika kikosi cha Arsenal dhidi ya Cardiff City wiki mbili zilizopita  Arsenal ilishinda mabao 2-1.

Emery  alimweka tena benchi  katika mchezo dhidi ya Manchester City  licha ya  Mhispania huyo  hudaiwa  kujali zaidi  uwezo wa mchezaji katika kila mchezo lakini hakutaka kuangalia alichokifanya Ozil dhidi ya Cardiff City.

 “Nadhani  ni suala gumu lakini sidhani kama  linausu kiwango cha mchezaji.Nafikiri Arsenal  wanataka kupunguza matumizi ya fedha na hiyo inaonekna kuwa na maana kwao,”anasema kiungo wa zamani wa Liverpool, Joe Cole.

 “Kwa miaka mingi Arsenal, ikiwa chini ya Arsene Wenger imekuwa na tabia kama hii.Kocha anatakiwa kutumia wachezaji bora alionao wakati anapowahitaji na Ozil ni mmoja kati ya nyota ndani ya kikosi.

“Kama utawauliza Alexandre Lacazette na Pierre-Emerick Aubameyanga kuhusu kucheza pamoja na Ozil watasema ndio wapo tayari, hivyo ni jambo la ajabu kumuona akiwa nje ya uwanja,”alisema.

Mkongwe wa Manchester United, Andy Cole anafananisha kitendo kinachomtokea Ozil sasa hivi ni kama mchezo wa kuigiza.

Ozil alikuwa katika afya nzuri ya mchezo kabla ya Arsenal kusafiri  kucheza michuano ya Ligi ya Ueropa ambao washika mtutu hao walifungwa bao 1-0 dhidi ya BATE Borisov  Alhamisi iliyopita.

“Huu ni mchezo wa kuigiza.Tunafahamu  uwezo wake,”anasema Cole.

Klabu ya Arsenal sasa ina haha kumtafutia Ozil timu ya kwenda kucheza kwa mkopo lakini mtihana wanaoupata ni ukubwa wa mshahara.

Arsenal kwa sasa haipo tayari kuendelea kumlipa  Ozil pauni milioni 18 kila msimu.

Ingawa Arsenal inafanya jitihada  za kumtafutia  Ozil klabu  kwa mkopo  lakini kiungo huyo wa  timu ya taifa ya Ujerumani  hataki kuondoka  kwa  mkataba wa muda mfupi.

Paris Saint Germain  ilitaka  kumsajili Ozil kwa mkopo wa muda mfupi  katika usajili mdogo wa Januari mwaka huu lakini alikataa.

Kinachotokea kwa  Ozil  akiwa Arsenal ndicho Emery alikuwa akikifanya dhidi ya Neymar  Jr pale PSG.

Emery na Neymar   walikuwa katika   mgogoro  uliotokana  na   nguvu aliyokuwa nayo Mbrazil  wakati akitua  PSG kwa dau la kuvunja rekodi.

Kinachotokea katika vyumba vya kubadili nguo timu ya Arsenal ni sehemu ya kilichokuwa kikitokea PSG   lengo likiwa kumfanya Neymar kukosa utulivu.

Emery  hataki kumpa   Ozil nguvu kubwa  ya ushawishi ndani ya klabu ya Arsenal  kama ilivyokuwa kwa Neymar katika klabu ya PSG.

Tayari  Emery amesema Ozil si mchezaji muhimu ndani ya kikosi cha Arsenal na wachezaji wengine wanahisi hataweza  kubadili uwamuzi wake kwa kuogopa  kuathiri  hali ya  hewa ndani ya  vyumba vya kubadili nguo ingawa nyota katika kikosi hicho wanaamini  wanamuhitaji Mjerumani huyo kwa sasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles