26.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 28, 2023

Contact us: [email protected]

Nandy: Mimi na Ruge tulipanga kuoana Machi mwaka huu

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Faustina Charles maarufu Nandy, ameweka wazi kwamba aliyekuwa Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group ambaye sasa ni marehemu, Ruge Mutahaba walikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na walipanga kufunga ndoa Machi mwaka huu.

Nandy amethibitisha hayo  katika mahojiano yake na mtangazaji, Millard Ayo jana Mei 13, 2019 kwamba walikuwa katika uhusiano wa kimapenzi na Ruge kwa miaka mitatu na walishatambulishana kwa wazazi wao wa pande zote mbili.

Amesema hawakutaka kuweka wazi mahusiano yao na kujulikana na watu hususani mitandaoni kutokana na namna walivyojipangia kuishi hivyo.

Amesema awali haikuwa rahisi kumkubali Ruge kwa sababu alishawahi kusikia mambo yake mengi na hata alipokuwa akimtumia meseji za kumuomba awe naye katika mahusiano alikuwa akijifanya hazioni ila baadaye alimkubali baada ya wawili hao kuonana na kuzungumza uso kwa uso.

Akizungumzia namna walivyoanzisha uhusiano wao Nandy amesema, “Nilikuwa napenda sana kumtumia kwenye mawazo yangu japo watu walikuwa wakimzungumzia kuwa mkali ila  alikuwa anapenda sana kunisikiliza na nilikuwa muwazi sana wa vitu vyangu hata vya ndani, nadhani ukaribu tuliotengeneza wa ‘kiboss’ na kiurafiki ndiyo ulitupelekea kuwa katika uhusiano,”.

Aidha Nandy amesema Ruge alikuwa ni zaidi ya mpenzi kwake aliishi naye kama baba na kaka yake na alikuwa akimshauri mambo mengi na mtu pekee aliyekuwa akimshauri katika mambo yake ya muziki na mambo binafsi hata wazo la kuwajengea wazazi wake nyumba lilitoka kwa Ruge.

“Katika kipindi ambacho Ruge alikuwa karibu na mimi na kunipa ujasiri ni wakati ambao video yangu na Billnass ilipovuja mitandaoni, nilikuwa sijazoea matusi ya mitandao ilinipa mawazo sana lakini alikuwa mshauri wangu mkuu.

“Baada ya ile video kusambaa yeye ndiyo alikuwa mtu wa kwanza kuonana na nilimpigia simu alivyopokea hata kabla sijaanza kuzungumza akaniambia najua kila kitu na tuko pamoja katika hili, tuliongea naye kwa simu alikuwa anatoka ofisini hadi akaja nilipokuwa hakukata,” amesema.

Aidha Nandy amesema kitu kikubwa kilichomvutia Ruge kwake ni jinsi anavyomcha Mungu kwa kuwa mara kwa mara alikuwa akimsisitizia kwenda kanisani hata kama yeye alikuwa haendi.

“Mimi kilichofanya nimpende Ruge ni mkweli na jinsi alivyokuwa ananiongoza katika maendeleo, nakumbuka wakati naanza kuwajengea wazazi wangu aliniambia nataka fedha yote ya kujengea hiyo nyumba niichume mwenyewe aliniambia anaweza kunisaidia lakini kuna leo na kesho inawezekana tukaachana au nisiwepo,” ameeleza Nandy.

Aidha Nandy amesema kwa kipindi ambacho Ruge hayupo duniani kinampa wakati mgumu kwani kuna wakati anatamani amtumie hata ujumbe wa simu ila anashindwa kuendelea kupata ushauri wake lakini hata hivyo bado anaendelea kuzitunza baadhi ya jumbe alizokuwa akitumiwa na Ruge enzi za uhai wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles