22.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Nandy aanika thamani ya mjengo wake

NA JESSCA NANGAWE

MWANADADA anayefanya vyema kwenye kiwanda cha burudani nchini, Faustina Mfinanga, maarufu kwa jina la Nandy ameweka wazi kuwa ametumia zaidi ya milioni 100 kukamilisha mjengo wake mpya.

Nandy ambaye kwa kiasi kikubwa muziki umeweza kumlipa amefunguka kuwa alikua akijibana ili kutimiza ndoto yake ya kumiliki nyumba baada ya kuwajengea wazazi wake.

Alisema pamoja na ugumu wa upatikanaji wa fedha kwa wakati mmoja lakini alikua akikusanya kile kidogo anachopata na kisha kupeleka kwenye ujenzi ambao ametumia muda mrefu kuujenga.

“Baada ya kuwajengea wazazi wangu na mimi nilitamani niwe na nyumba yangu, ilikua ni ndoto ya muda mrefu, nashukuru sasa imekamilika, nimetumia fedha nyingi zaidi ya milioni 100,” alisema Nandy.

Mbali na msanii Nandy, baadhi ya mastaa kwa sasa wameonekana kufanya maendeleo makubwa kupitia muziki wao kwa kumiliki nyumba zenye thamani kubwa kama vile Shilole, Shetta, Nay wa Mitego, Kitale na wengine wengi.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,502FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles