21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, August 16, 2022

Namna ya kuishi na watu wenye tabia ya kulaumu

Dk. Chris Mauki

HAKUNA hata mmoja anayependa kupokea lawama kila mara. Mara nyingi inategemea ni namna gani unavyomjibu yule anayekulaumu, labda utamwambia maneno ya dharau, kejeli, matusi au kujibu kihasira.

Kibaya zaidi ni kwamba majibu haya yote hayampoozi mlaumu, kinyume chake yana mpa moto wa kuendelea kulaumu, na hivyo hali kuwa mbaya zaidi.

Katika hali zote lawama zinapotolewa kuna kiwango fulani cha upande mmoja kuhisi kutotendewa sawa, ingawa mara nyingine lawama hizi huelekezwa kwa asiye mhusika. Wengi hupenda kuzirusha lawama kwa wale walio dhaifu kwao, mfano, baba kumlaumu mama, mama kulaumu watoto au wafanyakazi nk.

Mara nyingi ni ngumu kunyamaza pale unaporushiwa lawama, hususani pale unapojua kabisa kuwa lawama hizo hazikustahili wewe, katika hali kama hii yakubidi ujitahidi kukaa kimya, kwa sababu muhimu zifuatazo;

Kama wote mtafuka moto na kuwajeuri au kujibizana hakuna kitakachofanyika, hali itakuwa ngumu zaidi na mlaumu au mlalamishi atapata kitu kingine cha kulaumu juu yako, yamkini akasema wewe huambiliki

Kwa vyovyote lawama zitakavyokuwa, fahamu tu kuwa mteja (ikiwa ni kwenye biashara) wakati wote ana haki, fahamu hakuna biashara bila huyo mteja. Hata kama amekosa, mlaumu wakati wote hujiona ana haki ya kutoa malalamiko yake na kusikilizwa. Kwa kunyamaza na kumsikiliza, unatunza kazi yako na kuiendeleza.

Kama kelele hazitapungua, lawama zaweza kuvuka mpaka na kuwa lawama au shutuma binafsi nahii yaweza kuleta ugomvi binafsi.

Kwa sababu ni rahisi sana kupandishwa hasira zaidi ya kupooza hasira, ikiwa utamruhusu mlaumu akupandishe hasira, utalazimika kuzielekezea hata kwa watu wengine wasio husika, ambao unahitaji kuwapa huduma pia. Hii sio haki na inawapa mlango mwingine wa kuanza kukulaumu.

Ukiruhusu mtu akupandishe hasira, kiwango chako cha msongo wa mawazo kitapanda, na hivyo waweza kujikuta unapata matatizo kiafya. Mfano. Kuumwa kichwa mara kwa mara, mgongo kuuma, mshtuko wa tumbo, na mapigo ya moyo kuzidi kasi. BP, wale wenye vidonda vya tumbo huzidi kuuma nk.

Kuruhusu kupandiswa hasira mara kwa mara kazini, huwafanya wengi kwenda kuzishushia nyumbani, nah ii huleta mfarakano na watu wa kwenye familia. Hasira na migongano hii ikizidi nyumbani, kasi utalala na kuamka nayo na hivyo kwenda nayo kazini asubuhi, hii ukufanya kuanza siku na hasira na hivyo kukuaruzana na yeyote yule.

Unajua kabisa kuwa, sio jukumu lako kukasirikia kazini dhidiya mteja au wale unaowahudumia, hali hii ikitokea, utajihisi vibaya moyoni, na waweza wapoteza hata wale ulionao karibu na walio marafiki.

NINI TUFANYE KWA MTU MWENYE TABIA YA LAWAMA

Jitahidi kujiweka huru, mpole na asiyepaniki kwa vyovyote iwezekanavyo (be relaxed as possible) vuta pumzi ndefu, acha mabega na shingo yako iwe huru mbali na hasira na jaribu kuhisi utulivu.

Tulia hadi joto na moto wa mlaumu ushuke, ukijaribu kuweka neno hapa, atatulia na kukuamkia tena. Mwili wako uonyeshe mawasiliano, weka pozi la utulivu sio la shari, muangalie machoni, usimkwepe, kama ni kwenye meza, egemea kidogo upande wake kama vile uko tayari kumsikiliza kwa upole.

Msikilize anachosema sawia, ikiwezekana chukua karatasi na kalamu akuone ukiandika pointi za kile anachalaumu. Hii itakusaidia kumwonyesha kuwa unamaanisha na hivyo kushughulikia kile anacholaumu.

Pia itakukumbusha nini haswa kilikuwa kinalaumiwa mara baada ya yeye kunyamaza.

Baada ya kusikiliza anachokisema, mwonyeshe mlaumu kuwa unahisi sawa na vile anavyojisikia, na hata ingekuwa niwewe ungeumia au ungelaumu pia.

Mfano; Mwambie “Naelewa kabisa jinsi ilivyokuudhi hasa kwa jinsi ilivyotokea” hii inamwonyesha anayelaumu kuwa unamuhurumia na kwamba huoni kuwa analaumu tu bila sababu.

Pata muda wa kuliangalia tatizo kiundani, sio mara zote mlaumu ana haki, ingawa hauhitaji kumwambia hivyo usoni kwake. Kama ni jambo litakalohitaji muda basi mwombe muda wa kulishughulikia na muahidi kumpa taarifa baadaye na kweli ufanye hivyo ulivyoahidi. Pale unapogundua kuwa unamakosa katika lile lililokuwa lina laumiwa, basi kuwa mrahisi kuomba radhi na uwe mkweli usitake kufunika mambo na kujitetea.

Kamwe usijitetee, hatakama sio wewe mhusika mfano; “Sio kosa langu” mimi sikuwepo jana” kamwone bosi basi “Usilaumu kabla ya kuuliza kwanza” nk. Mlaumu hana muda wa kujua nani ni mhusika ili amlaumu yeye.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,814FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles