28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Namna ya kuepuka kutupa mabaki ya chakula

TAKRIBANI tani bilioni 1.3 za chakula hutupwa kila mwaka, hali ambayo huchangia kwa kiasi kikubwa mabadiliko ya tabia ya nchi.

Mabaki ya chakula ni moja kati ya matatizo makubwa yanayomkabili binadamu hii leo, limeeleza jarida la New York Chef Max La Manna.

Mwandishi wa makala za ‘More Plants, Less Waste’ anaeleza ni namna gani mtu anaweza kuleta mabadiliko.

“Chakula siku zote ni kiungo kikuu katika maisha yangu. Kuwa na baba mpishi, nilikuwa katika ulimwengu wa chakula.

Wazazi wangu wakati wote walinifundisha kutokutupa chakula. Duniani karibu watu milioni tisa, tunakabiliwa na tatizo la ukosefu wa chakula na zaidi ya watu milioni 820 hawana chakula cha kutosha.

Mabaki ya chakula ni tatizo kubwa linalomkumba binadamu leo hii – takribani theluthi moja ya chakula kinachozalishwa ulimwenguni hutupwa.

Kutupa chakula kunamaanisha kupoteza fedha, maji, nguvu, ardhi na gharama za usafirishaji.

Kutupa chakula pia kunaweza kuchangia mabadiliko ya tabia nchi. Chakula kilichotupwa ardhini huoza na kuzalisha gesi ya Methane.

Ili kuepukana na tabia hii inapaswa kufanya yafuatayo:

Nunua kwa malengo

Watu wengi hununua zaidi ya wanachohitaji.

Nunua kwa malengo kwa kuorodhesha mahitaji na kununua kilicho kwenye orodha.

Maliza chakula chote ulichonunua kwenye manunuzi yako ya mwisho sokoni kabla ya kununua mahitaji mengine.

Hifadhi vizuri chakula

Kutotunza vizuri chakula husababisha vyakula kutupwa. Watu wengi hawana uhakika wa namna wanavyoweza kutunza matunda na mbogamboga hivyo, kufanya viive hatimaye kuoza kabisa.

Kwa mfano, viazi, nyanya, matango na vitunguu havipaswi kuwekwa kwenye jokofu. Hivi vinapaswa kuwekwa kwenye chumba chenye joto kiasi.

Mashina ya mboga na mizizi inaweza kutumbukizwa kwenye maji.

Tunza chakula kinachobaki

Kiporo cha chakula si kwa ajili ya nyakati za mapumziko ya sikukuu pekee.

Ikitokea umepika chakula kingi na kikabaki, tafuta wakati wa kukila na kingine chochote kilichokusanywa kwenye jokofu.

Ni namna nzuri ya kuepuka kutupa chakula, zaidi ya hayo inasaidia kuokoa muda na fedha.

Kuwa rafiki na jokofu lako

Kugandisha chakula kwenye jokofu ni njia rahisi ya kukitunza.

Kwa mfano, mbogamboga ambazo kidogo ni laini zinazoweza kutumika kwenye kachumbari zinaweza kuwekwa kwenye mifuko au mikebe na kutumika siku nyingine kama kuchanganya na juisi na viungo vingine.

Kukifanya mbolea chakula kilichobaki ni njia nzuri ya kubadilisha mabaki ya chakula kuwa nishati ya mimea.

Licha ya kwamba si kila mtu ana nafasi kubwa ya mfumo wa kusindika mabaki, kuna mfumo rahisi ambao unaweza kumfaa kila mmoja ambaye hana sehemu kubwa ya kutosha.

Kurundika nje kunafaa zaidi kwa watu wenye bustani kubwa.

Hatua ndogo, matokeo makubwa

Hitimisho ni kwamba tunaweza kupunguza kiasi cha takataka na kuna namna mbalimbali za kufanya hivyo. Na kwa kufikiria kuhusu chakula unachotupa kila siku, unaweza kusaidia kuleta mabadiliko kwa kukitunza na kutunza mazingira.

Hata mabadiliko kidogo kuhusu namna unavyonunua, kupika na kutumia chakula kunaweza kupunguza athari kwa mazingira.

Kwa jitihada za bila kutumia nguvu, unaweza kupunguza kukitupa na kuokoa fedha, muda na kutunza mazingira.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,455FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles