23.8 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Nameless: Wahu ni mke sahihi kwangu

Nameless-David-Mathenge

NAIROBI, KENYA

MKALI wa muziki nchini Kenya, David Mathenge ‘Nameless’ ameweka wazi kuwa Wahu Kagwi ni mke sahihi katika maisha yake.

Msanii huyo amedai kuwa hadi sasa hakuna ambaye amemtuhumu mwenzake kwa kutoka nje ya ndoa, hivyo wanastahili kuwa katika ndoa hiyo.

“Nina miaka 11 sasa tangu nifunge ndoa na Wahu, naweza kusema kuwa huyu ni mwanamke sahihi kwangu kwa kuwa kila mmoja hakuna ambaye amemtuhumu mwenzake kutoka nje ya ndoa.

“Kupendana kunatufanya kila mmoja kumwamini mwenzake, huu ni mfano wa kuigwa kwa wasanii wengine pamoja na vijana wa sasa, lakini wengine wamekuwa wakifunga ndoa na baada ya muda wanaachana,” alisema Nameless.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,718FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles