26.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 17, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Naibu Waziri wa Nishati azindua namba mpya ya huduma kwa wateja wa TANESCO

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amezindua namba mpya ya bure ya huduma kwa wateja ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) – 180, huku akitoa maagizo matatu kwa wahusika kuhakikisha changamoto za wateja zinatatuliwa kwa haraka na kwa weledi wa hali ya juu.

Akizungumza Machi 12, 2025, jijini Dar es Salaam, Kapinga amesema kuwa namba hiyo imeboreshwa ili kuboresha huduma kwa wateja na kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika.

Akitoa maelekezo hayo Kapinga alisema jambo la kwanza ni wajibu wa kila mtoa huduma wa kituo hicho kuwa na majibu mazuri kwa wateja wanaopiga simu pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili.

“Wateja wanapopiga simu wanapaswa kutatuliwa changamoto zao kwa haraka, lakini pia muhakikishe wateja wanapata taarifa zinazohusu Tanesco kwa wakati kupitia ule utaratibu wakutatua changamoto husika ndani ya saa nne,” amesema Kapinga.

Pia amewataka viongozi TANESCO kukiangalia kituo hicho kwa ukaribu kwakuwafuatilia watumishi ambao watakuwa wanaenda kinyume na taratibu za kazi kuwachukulia hatua.

Akizungumzia kuhusu namba hiyo alisema uzinduzi wa namba hiyo utaongeza wateja watakaohudumiwa kwa simu kwakuwa mpaka Julai 2024 walipokea simu 1,500 kati ya 50,000 zilizopigwa.

Amesema anaamini kupitia namba hiyo 180 ambayo ni ya bure wanaamini idadi ya wateja watakaopiga simu itaongezeka kwakuwa namba za awali zilikuwa zikipigwa kwa Fedha.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Mhanidisi Gisima Nyamohanga amesema namba hiyo itaongeza wigo ya kutoa huduma na kuongeza idadi ya wateja watakaohudumiwa.

Alisema dunia ya sasa ya biashara ina ushindani wa kibiashara  unategemea uwepo wa huduma bora ya umeme na kutatua changamoto kwa wakati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
595,000SubscribersSubscribe

Latest Articles