28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

Naibu Waziri Nishati awaonya wakandarasi wazembe

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema serikali itaanza kuchukua hatua kwa  wakandarasi wazembe ambao wameshindwa kuendana na mikataba yao.

Judithi ameyasema hayo leo Disemba Mosi, 2023 jijini Dar es Salaam alipotembelea kituo cha kupoozea umeme Ilala kwa lengo la kuangalia uendelezaji wa mradi wa kuweka njia ya ardhini kutokea Ilala kwenda Kurasini.

Amesema moja  hatua za kukomesha  hali hiyo ni kuacha kuwaongezea mikata wakandarasi wazembe pindi inapomalizika.

Katika ziara hiyo amelitaka Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), kuhakikisha wakandarasi wanaopewa mikataba ya kusambaza vifaa vya kufanyia matengenezo kwenye njia za umeme wafanye kazi kulingana na mikataba yao.

“Niwaelekeze Tanesco hakikisheni mnatilia mkazo mikataba hiyo ili vifaa vipatikane kwa wakati,vifaa vimekua vinasumbua lakini hawa wasambazaji wengine ambao wapo kwa muda mrefu  na wanasumbu na  hawachukuliwi hatua tutaanza na wao,”amesema Kapinga.

Amesema kutokana na ukubwa wa mji wa Dar es Salaam pamoja na mahitaji yake endapo wahusika hawatachukuliwa hatua kwa kushindwa kutekeleza wajibu wao itaendelea kuleta athari kwa wananchi.

“Serikali imetoa fedha nyingi sana kwa hiyo hatutaweza kuvumili njia za umeme zisiboreshwe kwa sababu ya uzembe wa watu wachache tunapaswa kufanya kazi hizi kwa weledi ili watanzania waweze kuchagiza shughuli zao za kiuchumi,”amesema.

Akizungumza kuhusu uendelezaji wa njia ya ardhini ya umeme amesema mradi huo utakapo kamilika utaondoa shida ya kukatika kwa umeme kwenye maeneo ya Kigamboni, Ilala, Kurasini, Mbagala na Temeke kutokana na ongezeko la watu katika maeneo hayo.

Amesema wanaendelea na maboresho ya vituo vyao ikiwemo kituo cha kupozea umeme cha Mbagala ili kuhakikisha tatizo linaisha kabisa.

“Hata tukiwa na umeme wa kutosha lakini kama hatujaboresha njia za wananchi za kupata umeme wa uhakika basi bado tutakua na changamoto kubwa,”amesema.

Naye Mhandisi wa Mradi, Nicholas Anthony amesema mpaka sasa mradi umefikia asilimia 68.14 na unatarajiwa kukamilika Machi 2024.

Amesema mradi huo utakapokamilika utasaidia kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wilaya ya Temeke kwani maeneo hayo yatakuwa na uwezo wa kupokea umeme kutoka Ubungo,Kinyerezi,Kipawa kwenda Kurasini.

Mradi wa kusambaza njia za umeme ardhini kutoka Ilala kwenda Kurasini umefadhiliwa na serikali kwa asilimia 100.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles