27.7 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

Naibu Waziri azibana halmashauri kasi ndogo upandaji miti

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

NAIBU Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Khamis Hamza Khamis amezitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha zinatekeleza agizo la Serikali la kupanda miti milioni 1.5 kila mwakka ili kutunza, kuhifadhi mazingira na kulinda vyanzo vya maji huku akitahadharisha kuwa wasiotekeleza watawajibishwa.

Khamis ametoa wito huo Februari 25, 2023 wakati akiongoza shughuli ya upandaji miti katika Chuo cha Mtakatifu Agustino (SAUT), Mwanza inayotekelezwa na ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na vyuo vikuu nchini kupitia kampeni ya ‘Soma na Mti’ ambapo miti 270 ya vivuli na matunda imepandwa huku kampeni hiyo inalenga kutoa elimu na kuhamasisha wanafunzi kuanzia shule za awali mpaka vyuo kupanda miti

Amesema Serikali imeshaziwekea malengo halmashauri hizo kupanda miti milioni 1.5 lakini utekelezaji wake umekuwa wa kusua sua hivyo akazitaka kutekeleza mara moja agizo hili ili baada ya miaka mitano zitoke kwenye hali ya ujangwa huku akizitaka pia kulinda vyanzo vya maji kwa kuzuia utiririshaji maji yenye sumu na shughuli za kibinadamu zinazoharibu vyanzo hivyo.

“Naziagiza taasisi binafsi na za umma kupanda miti ya kutosha, vile vile taasisi za serikali na wananchi kuacha matumizi ya kuni na kuhamia kwenye nishati mbadala ili kupunguza ukataji miti. Mwanza ina vyanzo vingi vya maji lakini vimeharibika kwa sababu ya uchafuzi wa mazingira hasusab shughuli za binadamu,”

“Tutunze na kuhifahi mazingira kwa vitendo ili kukabiliana na athari za mazingira, programu hizi za upandaji miti zitaleta tija kubwa kwa sababu lengo ni wananchi wote hasa wanafunzi kuanzia chekechekea mpaka vyuo vikuu wapande miti,” amesema.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi amesema maelekezo waliyopewa na wizara yatatekelezwa kwa kasi kubwa kwani utunzaji mazingira ni moja ya kipaumbele chao na kazi hiyo itakuwa nyepesi kwani tayari wana kitalu chenye miche ya miti zaidi ya milioni moja.

“Tunao mpango kazi kwenye wilaya yetu na tutakwenda kutekeleza kwa kupanda miti milioni 1.5 na ifikapo mwakani idadi hii itafikiwa kwa sababu miti ipo ni jambo la kujituma tu na kushirikishana kuhakikisha agizo hili linatimizwa,” amesema Makilagi.

Naye, Meneja wa Wakala wa Misitu (TFS) Wilaya ya Nyamagana, Emmanuel Mgimwa amesema ili kutekeleza kwa vitendo utunzaji na uhifadhi mazingira wananchi wanapaswa kuanzisha mashamba madogo ya miche ya miti ambayo yatawasaidia nishati ya kuni, kilimo mseto na ufugaji nyuki.

“Ofisi yetu kwa kipindi cha Julai 2022 hadi Februari 2023 tumezalisha miche 97,310 na kugawa miche 32,970 ambapo tumewapa chuo cha SAUT miche 2,000 ikiwamo 270 ya matunda na vivuli ambayo imepandwa leo kwenye hii kampeni,” amesema Mgimwa.

Balozi wa Mazingira ofisi ya Makamu wa Rais, Mrisho Mabanzo, amesema kampeni ya ‘Soma na Mti’ iliyozinduliwa mwaka 2021 na Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango inalenga kuhamasisha wanafunzi kuona utunzaji mazingira na kupanda miti ni sehemu ya maisha yao, huku akiwaomba viongozi wa serikali kuwapa ushirikiano mabalozi hao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles