26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

NAIBU SPIKA AWAKUMBUSHA WABUNGE MASWALI YA KUMUULIZA WAZIRI MKUU

Maregesi Paul, Dodoma

Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, amewakumbusha wabunge kuwa na utaratibu wa kumuuliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa maswali ya kisera wakati wa maswali ya papo kwa hapo.

Kutokana na hali hiyo, Naibu Spika amemzuia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa asijibu maswali ya wabunge wa Chadema, Pauline Gekul wa Babati Mjini na Mbunge wa Tunduma, Frank Mwakajoka.

Amesema Waziri Mkuu akiulizwa maswali ya majimboni kwa wabunge hawezi kuyajibu kwa kuwa hawezi kujua kila kitu nchini.

Dk. Tulia ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma leo, alipokuwa akijibu mwongozo wa Gekul, aliyekuwa amemuuliza Waziri Mkuu swali kuhusu stendi ya mabasi ya Babati ambapo Naibu Spika, alimzuia Waziri Mkuu asilijibu swali hilo na la Mwakajoka aliyesema ameuliza swali la kisera.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,573FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles