24.8 C
Dar es Salaam
Friday, November 8, 2024

Contact us: [email protected]

Naibu Spika aimwagia sifa NSSF

       Na GUSTAPHU HAULE-PWANI

NAIBU Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, amelipongeza Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa hatua kubwa waliyofikia katika kuanzisha mafao mbalimbali ya kuikomboa jamii.

Hatua ya Naibu Spika kulipongeza shirika hilo ilikuja juzi katika maonyesho ya bidhaa za viwandani yaliyofanyika katika Viwanja vya Sabasaba, Kibaha, Mkoa wa Pwani, baada ya Meneja wa NSSF, Mkoa wa Pwani, Linus Bwegoge, kutoa ufafanuzi kuhusu fao jipya la kukosa ajira.

Katika maonyesho hayo, Bwegoge alimweleza Naibu Spika kuwa, NSSF wameamua kuanzisha fao jipya la kukosa ajira ili kuweza kuwasaidia Watanzania kutatua changamoto zao pindi wanapokosa ajira, iwe ni kwa kusimamishwa kazi au kumalizika kwa mikataba yao ya kazi.

Alisema kwamba, fao la kukosa ajira litamhusu mwanachama wa NSSF mwenye umri wa chini ya miaka 55, ambaye alichangia mfuko kwa muda wa miezi 18 na baada ya kusitishiwa ajira yake, atalipwa asilimia 33.3 ya mshahara aliokuwa akilipwa kazini.

“Lakini, mwanachama ambaye hakutimiza michango ya miezi 18, NSSF itaendelea kumsaidia kwa kumpatia mkopo wa asilimia 50 kufuatia kiasi alichochangia katika mfuko huo.

“Fao la kukosa ajira lililoanzishwa na NSSF limekuwa na maana kubwa kwa jamii kwa kuwa wengi wao wanakosa ajira, wanafukuzwa kazi na wengine mikataba yao ya kazi inamalizika.

“Kwa hiyo, pale mtu anapokosa ajira, NSSF wataendelea kumlipa mshahara mpaka atakapopata kazi,” alisema Bwegoge.

Kwa upande wake, Naibu Spika alisema kazi inayofanywa na NSSF ni kubwa na muhimu kwa kuwa inaelekeza nguvu katika kuwakomboa Watanzania na jamii kwa ujumla kulingana na vipato vyao.

Alisema kwamba, Serikali imeandaa mipango mizuri kwa ajili ya kuhakikisha kila Mtanzania anapata fursa ya kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii ikiwamo NSSF

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles