Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital
NAIBU Meya wa Manispaa ya Kinondoni wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Rwegasira Samson amezindua Data Base kwa ajili ya kuwasidia vijana wa Wilaya ya Kinondoni wenye taaluma mbalimbali.
Akizungumza Mei 13, alipokutana na viongozi mbalimbali na vijana wa chama hicho wakati wa uzinduzi wa data base Naibu Meya, Rwegasira amesema kuwa lengo ni kusaidia furusa mbalimbali kwa vijana.
“Halmashauri tupo na utaratibu wetu baada ya kukusanya mapato kutoka vyanzo mbalimbali huwa tunatoa asilimia 10 na tunagawa asilimia 4 kwaajili ya vijana kusaidia vijana wetu,” amesema Rwegasira.
Amesema kuwa nipo karibu na vijana ili kuwasaidia vijana furusa ambazo zipo kuna uchumi bahari utawasaidia vip?
“Kuangalia fursa za uvunaji majongoo wa baharini na kutoa elimu kwa vijana fursa zinazopatikana katika Uvuvi na tumemuomba Waziri wa Mifugo na Uvuvi amesema atatupatia boti 20 kwa ajili shughuli lazima tutumie mazingira kuwawezesha vijana,” amesema Rwegasira.
Nae Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Kinondoni (CCM), Abdul-Rahman Kassim amesema wamehitimisha ziara ya kata 20 katika Wilaya hiyo na wanafanya uzinduzi wa data base kuwatambua vijana na taaluma zao.
Amesema wanaamini wanaenda kuwaajiri vijana wa Kinondoni data base haichagui chama itasadia vijana wa vyama vingine kama Chadema, Cuf na vingine.
“Data base itasadia vijana katika ujasiliamari, sanaa na uvuvi hivyo Naibu Meya amefungua studio wenye vipaji watarekodi nyimbo zao bure hii furusa kwa vijana wa Wilaya Ya Kinondoni tuu,”amesema Kassim.