25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Nahodha TP Mazembe awaonya Simba Sc

Tima Sikilo, Dar es Salaam

Nahodha wa TP Mazembe, Rainford Kalaba, ambaye alivaana na kikosi cha Simba kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu wa 2011 amesema kikosi chao cha kesho ni tofauti na kile ambacho Simba wanakijua.

Akizungumza na Mtanzania Digital leo Ijumaa Aprili 5,  Kalaba amesema yeye ni miongoni mwa wachezaji waliokutana na Simba mwaka 2011 kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika hivyo Simba inapaswa kutambua kikosi cha sasa kina mabadiliko na anaamini mchezo wa kesho  hautakuwa rahisi.

Kabala amesema wanafahamu kwamba si rahisi kumfunga  Simba kwenye Uwanja wake wa nyumbani lakini wao kama wapinzani watapambana kuona wanapata matokeo mazuri dhidi yao.

“Tumefurahi kufika hatua ya robo fainali na kila mchezaji atapambana ili kufanikisha kufika hatua ya nusu fainali, kuwa kwenye michuano hii ni faida kwa kila timu na nchi yake hivyo tusubiri tuone matokeo,” amesema Kabala

Kalaba na Emmanuel Okwi ndiyo wachezaji pekee wa vikosi hivyo ambao watakutana kwa mara ya pili kwenye mchezo huu kutoka miaka nane iliyopita timu hizo zilipokutana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,430FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles