24.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Nahodha Polisi azungumzia bao la Bocco

Theresia Gasper – Dar es salaam

BAADHI ya wachezaji wa Polisi Tanzania wamezungumzia  bao walilofungwa na mshambuliaji wa Simba, John Bocco, wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo, Polisi ilikubali kipigo cha mabao 2-1.

Mabao ya Simba yalifungwa na Bocco na Ibrahim Ajib, huku lile la Polisi likikwamishwa wavuni na Sixtus Sabilo.

Wakizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, wachezaji hao walipinga bao hilo kwa madai kwamba halikuwa halali.

Nahodha wa Polisi, Iddy Mobby, alisema mchezo ulikuwa mzuri kwani tangu mechi inaanza wao ndio walikuwa wanamiliki mpira kwa asilimi kubwa lakini baada ya bao la Bocco wanaloamini lilikuwa lakuotea walipoteana..

“Tulitoka mchezoni mara baada ya bao la Bocco kwani lilikuwa ni la kuotea kabisa, hali iliyotufanya litutoe mchezoni na morali kupungua,” alisema.

Alisema kwa sasa wanahamishia akili zao katika maandalizi ya mchezo wao ujao dhidi ya Coastal Union,  ambao hawatahitaji kingine zaidi ya pointi tatu.

Kwa upande wa Hassan Maulid, aliwataka  mashabiki wao kukubaliana na matokeo kwani  soka ndivyo lilivyo pale timu mbili zinazposhindana lazima mshindi apatikane.

“Hatuwezi kumlaumu refa wa kati kwa lile bao la Bocco kwani inawezekana hakuona vizuri, lakini mshika kibendera ndio alitakiwa atoe uamuzi, tunaiomba Bodi ya Ligi iangalie suala hili vizuri ili tuweze kuendeleza mpira wetu,” alisema.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,538FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles