30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Nahodha Gwambina adai hawajatoka relini

NA MWANDISHI WETU-MWANZA

NAHODHA wa timu ya Gwambina ya Misungwi mkoani Mwanza, Jacob Massawe, amesema kichapo walichopata kutoka kwa Ruvu Shooting hakijawavunja moyo, badala yake wataendelea kupambana ili wapate matokeo change kwenye michezo yao ijayo.

Gwambina ambayo ni miongoni mwa timu tatu mpya katika Ligi Kuu Tanzania Bara, nyingine, Ihefu na Dodoma Jiji, ilikumbana na kipigo hicho katika mchezo wa ligi hiyo uliochezwa juzi Uwanja wa Mabatini, Pwani.

Lakini kabla ya hapo, Gwambina ilizikabili Kagera Sugar na kulazimishwa suluhu pamoja na Biashara United, ambapo ilipoteza kwa kucharazwa bao 1-0, Uwanja wa Karumbe mjini Musoma.

Hii ina maana kwamba, timu hiyo haijafanikiwa kuonja radha za ushindi tangu ilipoingia kwenye mikiki mikiki ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Akizungumza na MTANZANIA jana Massawe alisema kuwa, wamejifunza kitu kupitia matokeo mabaya waliyoyapa katika michezo yao iliyopita na sasa wamejipanga kuhakikisha wanavuna pointi tatu katika mchezo wao ujao dhidi ya Simba.

“Mpira una matokeo yake ya ajabu, hakuna namna zaidi ya kukukubali tumeshindwa na kujipanga upya kwa ajili ya mechi zetu zinazofuata.

“Hakuna mchezaji ambaye anapenda kuona timu inashindwa lakini kwa kuwa hata wapinzani wetu nao wanajipanga kama sisi ndio maana matokeo yanapatikana uwanjani.

“Hatujapoteza matumaini, bado tuna nafasi ya kufanya vizuri, mashabiki waendelee kutupa sapoti kwani timu ina maelewano makubwa na hakuna tatizo lolote ni mpira tu,” amesema. 

Gwambina itakuwa mwenyeji wa Simba, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaochezwa Jumamosi hii Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles