25.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 22, 2024

Contact us: [email protected]

Nadal, Keber waanza vema US Open

Rafael Nadal
Rafael Nadal

NEW YORK, MAREKANI

BAADA ya kufanya vibaya katika michuano ya tenisi nchini Brazil kwenye Olimpiki, nyota kutoka nchini Hispania, Rafael Nadal, ameanza vema katika mchezo wake wa kwanza wa michuano ya wazi ya nchini Marekani.

Nyota huyo ameanza kwa kumchapa mpinzani wake, Denis Istomin kwa seti 6-1, 6-4, 6-2. Nyota huyo amedai kuwa anafurahi sana kwa kuanza vizuri katika michuano hiyo mikubwa.

“Hii ni dalili ya kuja kufanya vizuri katika michuano hii, ninaamini nitakutana na upinzani mkubwa, lakini nitafanikiwa kufanya vile ambavyo nimekusudia, nimepoteza baadhi ya michuano mikubwa kwa siku za hivi karibuni, lakini michuano hii nitahakikisha ninaondoka na ubingwa huo,” alisema Nadal.

Hata hivyo, kwa upande mwingine nyota wa mchezo huo kwa upande wa wanawake, raia wa nchini Ujerumani, Angelique Kerber, alifanikiwa kumchapa mpinzani wake, Polona Hercog kwa seti mbili 6-0 1-0.

Wakati huo bingwa mwingine, Garbine Muguruza naye alianza vizuri kwa kumshinda mpinzani wake, Elise Mertensi kwa 6-0 6-3. Mshindi wa michuano ya Olimpiki, Monica Puig, raia wa nchini Puerto Rico, ameanza vibaya kwa kupokea kichapo kutoka kwa mpinzani wake, Zheng Saisai, raia wa nchini China kwa seti 6-4 6-2.

Hata hivyo, Monica amedai kuwa anahitaji kupumzika, hasa baada ya kutumia nguvu nyingi kwenye michuano ya Olimpiki nchini Brazil.

“Siku zote hakuna mashindano madogo, ninaamini kila mmoja amekuja kwenye michuano hii kwa ajili ya kuchukua taji, hivyo lazima kutakuwa na upinzani mkubwa, sishangai kuanza vibaya kwa kuwa nilikuwa kwenye Olimpiki, ninastahili kupata muda wa kupumzika ili kuweka sawa mwili wangu,” alisema Monica.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles