30 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

Nacte yavifutia usajili vyuo 10

Brighiter Masaki -Dar es salaam

BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte), limevifutia usajili vyuo 10 kwa kushindwa kufuata utaratibu na kutokidhi vigezo vinavyotakiwa na baraza katika utoaji wa mafunzo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Mkurugenzi Udhibiti, Ufuatiliaji na Tathmini Nacte, Dk. Jofrey Oleke, alisema hatua hiyo inatokana na ukaguzi uliofanyika kati ya Oktoba na Desemba mwaka jana katika vyuo 105 na kubaini 10 vina upungufu mbalimbali.

Oleke alisema baraza linazingatia mambo mbalimbali katika usajili wa vyuo ikiwamo uwepo wa walimu wa kutosha, vitendea kazi, uwezo wa kuendesha chuo na maabara na kulazimika kufuta usajili baada ya kubaini kuna upungufu katika vyuo hivyo.

“Baraza limefutia usajili vyuo saba baada ya kubaini mapungufu mbalimbali, kabla ya kuvifutia vyuo hivyo baraza liliviandikia barua ya kuhakikisha vinarekebisha changamoto zilizobainishwa wakati wa ukaguzi ili viendelee kuwa na sifa ya kutoa mafunzo, hata hivyo vyuo hivyo havikutii maagizo halali ya baraza.

“Vyuo hivyo ni pamoja ERA Training College Bukoba, Azania College of Management Dar es Salaam, Time School of Journalism Dar es Salaam (TSJ), Clever College Dar es Salaam, Aces College of Science (ACES) Mwanakwerekwe, Zanzibar, Zanzibar Institute of Business Research and Technology (ZIBRET), Gender Training Institute, Dar es Salaam,” alisema Dk. Oleke.

Aidha alisema kuwa vyuo hivyo havikutii maagizo halali ya baraza na tayari vimeshapewa barua ya kuarifiwa kuhusu uamuzi huo.

Nacte imewataka wanafunzi waliokuwa wakisoma kwenye vyuo hivyo kuhamishwa mara moja na kupelekwa katika vyuo vinavyoa mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na vyuo husika ili waweze kuendelea na masomo yao.

Dk. Oleke alisema mbali ya vyuo hivyo saba, vingine viwili viliomba kusitisha kutoa mafunzo kwa sababu mbalimbali ikiwamo uwezo wa kifedha.

“Vyuo viwili ambavyo ni College of Business and Management cha Dar es Salaam na University Computing Centre (UCC) Mwanza Campus, viliomba kusitisha mafunzo kwa sababu mbalimbali zikiwemo uwezo wa kifedha wa kugharamia mafunzo.

“Chuo kingine kimoja, Kizimbani Agricultural Training Institute – Zanzibar kimekuwa sehemu ya Chuo Kikuu cha Zanzibar – State University of Zanzibar (SUKA) hivyo Baraza limefuta usajili wa chuo hicho.

“Baraza linapenda kutangazia umma kuwa limefuta usajili wa vyuo 10 baada ya kushindwa kufuata taratibu zinazoendana na matakwa ya usajili wa vyuo hivyo,” alisema Dk. Oleke

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,968FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles