32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

NACTE yapiga kofuli vyuo vitano

Steven MloteJOHANES RESPICHIUS NA WILLIAM BAZOMBANZA, DAR ES SALAAM

BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limevifutia usajili vyuo vitano kuendesha mafunzo, huku vingine 41 vikigundulika kuendesha mafunzo bila kusajiliwa.

Tamko hilo lilitolewa Dar es Salaam jana na   Mwenyekiti wa NACTE,   Steven Mlote, alipozungumza na waandishi wa habari.

Alisema Baraza limefikia uamuzi huo baada ya kutembelea na kukagua vyuo mbalimbali na kubaini   upungufu ambao umesababaisha kufutiwa usajili na vingine kufungiwa kwa muda.

Alivitaja vyuo vilivyofutiwa usajili kuwa ni   State College of Health and Allied Sciences, Zoom Polytechnic College, Tabitha College, Financial Training Centre na TMBI College of Business and Finance, vyote vya Dar es Salaam.

“Vyuo hivyo vimebainika kuwa vinaendesha mafunzo kwenye mazingira yasiyostahili na pia vina upungufu mwingi katika uendeshaji mafunzo, hivyo kupoteza sifa za usajili,” alisema.

Alisema Baraza lilifuatilia na kutathmini uendeshaji wa mafunzo katika vyuo vilivyopo chini ya NACTE na kugundua   vipo vyuo 41 ambavyo havina usajili na vinatoa mafunzo bila kibali,” alisema.

Mlote alisema vyuo hivyo 41 vinavyotoa elimu ya ufundi bila kusajiliwa kwa mujibu wa sheria, vimepewa   wiki mbili na kutakiwa vijisajili mara moja kwenye Baraza hilo kabla ya kuchukuliwa hatua kali za  sheria.

Alivitaja vyuo hivyo kuwa ni King Solomoni College – Arusha, Avocet College of  Hotel Management – Arusha, Kewovac Nursing Training Centre – Mbagala, Dar es Salaam, St. Family Health Training Institute – Mbagala, Dar es Salaam, Bethesda Montessori Teachers Training College – Arusha, Green Themi Teacher’s College & Green Themi Institute of Tourism.

Vingine ni Mainland Institute of Professionals – Arusha, St. David College of Health – Dar es Salaam, Islamic Culture School – Dar es Salaam, Tanzania Education College – Dar es Salaam, Macmillan Training College – Dar es Salaam, Tanzania International University (TIU) – Dar es Salaam

Pia vimo  Dodoma College of Business Management – Dodoma, Faraja Health and Emergencies – Mbeya, St. Joseph College – Mbeya, St. Peter Health Management – Mbeya, Kapombe Nursing School – Mbeya, Uyole Health Institute – Mbeya, Josephine Health Institute – Mbeya, Institute of Public Administration – Chake chake Pemba, Dar es Salaam College of Hotel and Business Studies – Vuga, Unguja, Zanzibar and Chake Chake, Pemba, Zanzibar.

Vyuo vingine ni Zanzibar Training Institute, the Professional College of Information Technology, Languages and Business Studies – Mwera Meli Sita Unguja  Zanzibar, Azania College of Management – Raha Leo, Zanzibar, Time School of Journalism – Chakechake, Pemba, Residence Professional College – Mombasa, Zanzibar na   Mkolani Foundation Organisation – Mwanza.

Pia alivitaja Kahama College of Health Sciences – Kahama, Institute of Adult Education-Mwanza Campus – Luchelele Site, Zoom Polytechnic – Bukoba, Johrow Star Training College – Shinyanga, St. Thomas Training College – Shinyanga na Dar es Salaam School of Journalism and Mass Communication DMSJ – Bukoba.

Adhabu hiyo imegusa pia Dar es Salaam School of Journalism and Mass Communication (DMSJ – Mwanza, Dar es Salaam School of Journalism and Mass Communication (DMSJ – Geita , Dar es Salaam School of Journalism and Mass Communication (DMSJ – Simiyu, Harvest Institute of Health Sciences – Mwanza, Singin International – Bukoba, College of Business Management – Mombasa, Zanzibar, Tanzania Star Teachers College – Chakechake, Pemba, Zanzibar, Tanzania Star Teachers College – Unguja, Zanzibar na St. Mary’s International School of Business – Sumbawanga.

Alisema Baraza   limetoa notisi ya kuvishusha hadhi  vyuo 11  nchini kutokana na kutoa programu zisizo na kibali ingawa vimesajiliwa.

Vyuo hivyo  ni pamoja na University of Africa ambacho kinatoa programu ya usimamizi wa biashara, uuguzi, uwakala wa forodha na nyingine.

“Pia Baraza linavitaka vyuo 112 ambavyo vimegundulika kuwa hadhi ya usajili imekwisha muda wake, ndani ya mwezi mmoja kuanzia sasa, viwe vimerekebisha hadhi hizo ndipo viruhusiwe kuendelea kutoa mafunzo.

“Baadhi ya vyuo hivyo ni Mteule Training College, Eagle Wings Training College, Green Hill Institute (GHI), Zanzibar Institute of Journalism and Mass Communication (ZIJMC), VETA Kipawa Information and Communication Technology,” alisema    Mlote.

Alisema Baraza hilo limebaini vyuo 52 ambavyo hadhi ya ithibati imefikia ukomo na hamna hatua zozote zilizochukuliwa, hivyo vimepewa mwezi mmoja kurekebisha kasoro hizo ndipo viendelee na mafunzo.

Mlote aliwataka wanafunzi ambao vyuo vyao vimefungiwa kuwasiliana na Baraza hilo ili kuhamishiwa kwenye vyuo vingine vyenye sifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles