33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

NaCoNGO yapata viongzi wapya

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

BARAZA la Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali (NaCoNGO) limepata viongozi wapya huku Mwenyekiti mpya wa Baraza hilo, Lilian Badi  akiahidi kuyatekeleza yale ambayo aliyaahidi  wakati akiomba kura.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo,leo Julai 8, 2021,Mwenyekiti wa Kamati ya mpito iliyosimamia uchaguzi huo,Flaviana Charles amemtaja Badi kuibuka na ushindi mara baada ya kupata kura 21 huku Jane Magigita akiambulia  kura 8.

Katika nafasi ya Katibu Mkuu,wajumbe hao wamemchagua, Revocatus Sono kwa kura 22 huku Gifti Kilasi akiambulia kura 7.

Nafasi ya Mwekahazina wajumbe hao wamemchagua John Kiteve kwa kura 15 huku Miraji Malinda akipata kura 13 na nafasi ya Kamati ya  Fedha na Utawala wajumbe hao wamempigia kura za ndio Gaidon Haule ambaye alikuwa peke yake katika nafasi hiyo.

Katika kamati ya maadili wajumbe hao wamemchagua Novatus Marandu ambaye amepata kura 15 na Kamati ya Maendeleo na Uwezo akichaguliwa Rhobi Samweli,Kamati ya Utandaa na Mawasiliamo akichaguliwa Asifiwe Mallya  huku wajumbe wanne wa Bodi wakiwa ni Jane Magigita,Revocatus Sono,Paulina Majogoro na Baltazari Komba.

Akizungumza mara baada ya kutangazwa  kwa matokeo Mwenyekiti mpya Baraza hilo,Badi  ameomba ushirikiano huku akiahidi kutekeleza yale ambayo aliahidi wakati wa kuomba kura.

“Mengi tumezungumza  tumetoa ahadi nyingi kwa pamoja tutaenda kuyafanyia kazi  yale tuliyoaahidi kikubwa naomba ushirikiano,”amesema.

Kwa upande wake,Katibu mpya wa Baraza hilo,Sono amewashukuru wote waliomwamini kwa kumpigia kura ambapo amedai kwamba mchakato huo haukuwa mdogo.

Naye,Mwekahazina mpya Kiteve amesema watakuwa wasiri wa vikao kwa kutokutoa siri huku akidai kwamba watatoa ushauri sahihi kwa viongozi wa juu.

“Tutaendelea kumshauri Mwenyekiti pamoja na wengine tutakupa ushauri unaofaa (Mwenyekiti) sisi hatutoi siri na tutakuwa wasiri wa vikao,’’amesema.

Naye Mbunge wa Viti Maalum kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira amewataka viongozi wapya kutokufanya kazi kwa kificho na  badala yake wanatakiwa kuwa wawazi katika mambo yao pamoja na kufanya kazi kwa bidii ili waweze kuonekana.

Pia,amewataka kuwa wawakilishi wa NGOs zote kubwa na ndogo bila ya kuweka matabaka huku akisisitiza uchaguzi umeisha sasa ni wakati wa kuchapa kazi.

“Uchaguzi umeisha sasa tuwe pamoja.Rai yangu kamati ya mpito iendelee kuwa walezi wa hawa viongozi wapya,”amesema.

Naye,Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali,Dk.Richard Sambaiga amewataka viongozi hao wapya kufanya kazi kwa tija,kuimarisha uhusiano wa NGOs ndani ya sekta huku akidai Bodi  itatoa ushirikiano kwa baraza hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles