25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

Nabii: Watanzania tuungane kuliombea taifa

Beatrice Kaiza

Waumini wa dini zote watakiwa kuliombea Taifa la Tanzania ili kuepuka majanga.

Wito huo umetolewa na mtumishi wa Mungu, Nabii Joshua ambapo amesema wakati mwengine taifa linapofikwa na majanga yanayohatarisha maisha ni muhimu waumini wote kuungana na kuwa kitu kimoja ili kuliombea taifa kuepuka majanga na maafa.

“Tumeungana kwa pamoja kuwaombea watu wa Moshi kwa kupoteza ndungu zao huu ni msiba wa taifa lakini kwa uwezo wa Mungu ametupa wasaa wa kumshukuru  kwa kila jambo na kumuomba amani,” amesema Nabii Joshua.

Amesema Watanzania wanatakiwa kuitumia amani kama tunu ili kujipatia maendeleo.

“Amani haiwezi kudumu pasipo kumuomba Mungu aendelee kutujaalia amani hiyo, waumini wote tuungane tuombe Mungu ili pasitokee mtu, kikundi kitakachoweza kuvuruga amani hii tuliyoachiwa na mababu zetu,” amesema Nabii Joshua.

Hata hivyo amempongeza Rais John Magufuli kwa kuendelea kutetea wanyonge na kuimarisha uchapakazi hasa kwa vijana.

“Rais Magufuli ni Kiongozi wa kipekee anaependa usawa kwa watu wote ndio maana anaitwa rais wa wanyonge hivyo tumuunge mkono na tumuombee pia kwa maana kazi anayofanya sio ndogo hasa linapokuja suala la kuliongoza Taifa,” amesema Nabii Joshua.

- Advertisement -
bestbettingafrica
Previous articleMaafa kwa Mwamposa
Next articleSimanzi yatawala Moshi

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,301FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles