30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 19, 2021

Nabii Joshua awataka Watanzania wamrudie Mungu

Na Mwandishi Wetu-MOROGORO

KIONGOZI Mkuu wa Huduma ya Sauti ya Uponyaji Tanzania, Nabii Joshua Aram Mwantyala, amewataka Watanzania kuendelea kujinyenyekeza kwa Mungu kwa kuwa anaenda kuachilia uponyaji kwa taifa muda wowote.

Wito huo aliutoa Kihonda mjini Morogoro, muda mfupi baada ya kuongoza maombi mfululizo ya kuliombea taifa ili Mungu akaliponye dhidi ya virusi vya corona na changamoto mbalimbali linalokabiliana nazo kwa sasa.

Nabii Joshua alimwomba Mungu azidi kuwapa viongozi wakiongozwa na Rais Dk. John Magufuli, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais, Samia Suluhu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na viongozi wengine moyo wa ujasiri na afya njema ili wazidi kuwatumikia Watanzania kwa moyo wa upendo.

 “Ukisoma Bibilia Takatifu kitabu cha pili Mambo ya Nyakati 1:14 inaeleza kwa kina kuwa ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu watajinyenyekeza, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi zao, na kuiponya nchi yao.

“Katika hiki kitabu cha Mambo ya Nyakati, tumeona namna ambavyo ukuu wa Mungu una nguvu ya kubadili kilichoonekana hakiwezekani kuwezekana, kubadili mateso kuwa furaha, kuiponya nchi kutoka katika magonjwa mbalimbali kama maambukizi ya virusi vya homa kali ya mapafu ya corona (Covid-19) na mengine mengi, ninaamini uponyaji unaenda kutokea muda wowote kwa taifa letu,” alisema Nabii Joshua.

Mbali na hayo, alisema kila Mtanzania katika kipindi hiki ambacho wanaendelea kumwomba Mungu, aendelee kuzingatia miongozo na kanuni zinazotolewa mara kwa mara na Serikali kuhusu namna ya kujikinga na virusi hivyo.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,848FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles