25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Mzungu Kichaa: Jina nilipewa na Juma Nature

Glory Mlay

MSANII wa bongo fleva, Espen Sorensen ‘Mzungu Kichaa’ amesema jina hilo la utani alipewa na Juma Nature baada ya kuingiza kiitikio cha wimbo wake wa Hili Game.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mzungu Kichaa alisema wakati anaingiza kiitikio kwenye wimbo huo alikuwa anakosea sana, hivyo Juma Nature ndipo alipomwambia kuwa yeye atakuwa Mzungu Kichaa.

“Kuniita Mzungu Kichaa haimaanishi kuwa nimevurugwa hapana, nilikosea nikawa naimba maneno mengine tofauti na ndipo akaniambia kuwa wewe Mzungu Unakichaa, jina likaanzia hapo kwa kuwa nilikuwa sieleweki,” alisema.

Aliongeza kwa kusema, hakuchukia baada ya kupewa jina hilo na ndio maana akakubali kuitwa hadi sasa.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,522FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles