29.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 30, 2024

Contact us: [email protected]

Mzozo wa umiliki wa rangi ya chama waibuka Uganda

KAMPALA, UGANDA

VYAMA viwili vya upinzani nchini Uganda vinazozana juu ya haki ya kutumia rangi nyekundu, kila chama kikidai kuwa ndicho kina haki ya kuitumia rangi hiyo kama utambulisho wake.

Chama kikongwe cha UPC kinaungwa mkono na Tume ya Uchaguzi nchini humo, kinadai kuwa chama kipya cha NUP kinachoongozwa na msanii Bobi Wine kilikosea kuanza kutumia rangi ambayo imekuwa yao kwa miaka mingi.

Lakini NUP imekanusha madai hayo ikisema imetumia rangi hiyo ikiwa vuguvugu la ‘People Power’ na hakuna aliyejitokeza kupinga hadi pale waliposajiliwa kama chama.

Rais wa chama cha UPC, Jime Akena ambaye ni mtoto wa mwasisi wa chama hicho, Milton Obote anasema rangi nyekundu ni ya UPC tangu miaka 60.

Huku mwanasheria wa vuguvugu za ‘People Power’ Asumani Basalirwa ambaye pia ni rais wa chama cha upinzani cha JEEMA anapinga tuhuma za chama kikongwe cha UPC:

Hata hivyo, Tume ya uchaguzi ndiyo itatoa maamuzi ya mwisho kwa vyama hivyo viwili ni kipi kitatumia rangi nyekundu katika nembo yao kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2021.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles