30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mzimu wa ajabu waanua unga wa ugali

flour

Na Ibrahim Yassin, Rungwe

WANANCHI  wa Kijiji  cha  Mwela  Kata  ya  Kandete  wilayani  Rungwe Mkoa wa Mbeya wako hatarini kukumbwa na baa la njaa baada ya kuibuka kile kinachodaiwa ‘mzimu wa ajabu’ ambao umekuwa ukianua unga  unapokuwa umeanikwa juani na kupotea hewani katika mazingira ya kutatanisha.

Hali  hiyo  imejitokeza  siku  chache baada ya ‘mzimu’ huo kuzuka  katika kijiji hicho   ikielezwa kuwa unga na mazao mengine yaliyokuwa yameanikwa juani yalipotea hewani.

Kutokana na tukio hilo,   imewalazimu wananchi wa Kijiji cha Mwela kutisha mkutano wa halmashauri ya kijiji   kujadili na kutafuta suluhu ya hali hiyo.

Akizungumza na mwandishi   kuhusu tukio hilo, mkazi mmoja wa kijiji hicho, Hamfrey Mwakitwange, alisema kuibuka kwa mzimu huo kumezua hofu kwa wakazi wa Mwela na maeneo ya jirani.

Alisema   mwaka huu kuna hatari ya kutokea  ukame na  baa la njaa    baada ya kuibuka   mzimu huo wa ajabu.

“Kwa tukio la kuwapo   mzimu huu wa ajabu tumejawa na hofu kubwa   na kuna dalili ya kukumbwa na baa la njaa mwaka huu.

“Mzimu umekuwa ukichukua chakula hasa unga na mazao yanayoanikwa juani…tunabaki tunajiuliza, na sasa kimeitishwa kikao cha halmashauri ya kijiji ingawa mtazamo umegawanyika… sasa kuna wengine wanataka hata tuhushishe waganga,” alisema Mwakitwange.

Mjumbe wa Nyumba 10 wa CCM, Matrida Mwaisumbwa, alisema   kitendo cha kuibuka   mzimu huo ambao umekuwa ukichukua chakula,  umeleta sintofahamu kijijini hapo.

Alisema   hata wanapokuwa wanapika chakula kama ugali au ndizi, kimekuwa hakina radha   na inadaiwa chakula hicho pia kinakuwa kimetembelewa na mzimu huo wa ajabu.

Alisema uongozi umeandaa mkakati wa kupita nyumba kwa nyumba   kukusanya michango  kuwasaidia wananchi ambao wamekwisha kuathirika na mzimu huo.

Hata hivyo,  Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwale, Ferki  Mwandenga, alisema licha ya kuwapo taarifa za mzimu huo wa ajabu  anashindwa kuieleza kwa kina hali hiyo.

“Siwezi kulisema hili jambo maana linachanganya kidogo, sijui ni tukio la kichawi? Ingawa pamoja na hali hiyo, tambua kuwa Serikali haiamini uchawi,” alisema Mwandega.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles