26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

MZEE MWINYI ATOBOA SIRI YA AFYA YAKE

mwinyi

NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

RAIS mstaafu, Mzee Ali Hassan Mwinyi, amesema siri kubwa ya afya aliyonayo ni kuzingatia utaratibu wa kufanya mazoezi ya kutembea na kuendesha baiskeli.

Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana wakati wa ufunguzi wa kampeni ya kufanya mazoezi kitaifa ili kupambana na magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza.

“Kila siku nafanya mazoezi ya mwili kwa dakika 90, ikiwamo kutembea na kuendesha baiskeli ya ndani,” alisema.

Pia alisema wengi humshangaa kuwa licha ya umri mkubwa alionao, lakini bado anaonekana kuwa na afya njema.

Kauli hiyo ya Mzee Mwinyi imekuja siku chache tangu Rais Dk. John Magufuli kueleza kwamba siri ya afya ya kiongozi huyo wa zamani, ni kuwa na wake wawili lakini mwenyewe aliitafsiri kuwa ni utani.

“Mimi ni mkubwa kwa wengi wenu hapa (washiriki wa matembezi), hata mara tatu, lakini nashukuru nilikuwa nikiweza na sasa naweza, matumaini yangu nitaendelea kuweza. Marafiki zangu waliniuliza wengine wananitania, nawezaje kuwa mzima namna hiyo kwa mtu mwenye umri mkubwa kama wangu, hata Rais Dk. Magufuli alinitania… lakini mambo haya hayataki dawa, mazoezi ni jambo la maana, ni jambo linalostawisha mwili, mkitaka kujua faida ya mazoezi niangalieni mimi,” alisema Mwinyi.

Alisema alibahatika kufanya kazi na Mwalimu Julius Nyerere, na kwamba alikuwa mwalimu mzuri ambaye hana mfano kwa sababu wakati mwingine alikuwa hana haja ya kutoa maneno bali mwenendo wake ulifundisha.

“Mwalimu mzuri ni yule anayefanya mwenyewe, vijana sina haja kuwaambieni kwamba mazoezi ni jambo jema, niangalieni nilivyo mtafundishika. Acheni kula vyakula vyenye mafuta mengi, mtu mmoja akanishangaa kuona nasoma bila kutumia miwani, nimewaambia natumia dakika 90 kila siku kwa mazoezi, matokeo yake sijambo, mkifanya mazoezi kiukweli mtaona manufaa,” alisema Mwinyi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles