20.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 28, 2022

Mzee Jangala: Nilitaka mwanangu awe mwanajeshi

jangala23NA CHRISTOPHER MSEKENA

MKONGWE wa filamu za vichekesho nchini, Bakari Mbelemba maarufu kama Mzee Jangala, amesema alitamani mwanaye wa kwanza wa kiume awe mwanajeshi badala ya kuwa kwenye fani yake ya sanaa.

Mzee Jangala alisema enzi zao walikuwa wanaamini zaidi ukiwa na mtoto mwanajeshi kuna mambo mbalimbali atakuwa anaweza kuyatimiza kama atakuwa na nafasi kubwa.

“Chaguo la kwanza nilitaka mwanangu awe mwanajeshi, kama alikuwa anataka kuwa daktari au kufanya sanaa basi nilipenda avifanye akiwa jeshini lakini ilikuwa tofauti kwani baada ya kumaliza kidato cha nne akakataa jeshi,” alisema Jangala.

Aliongeza kuwa baada ya mtoto wake kumjibu hivyo hakuwa na uwezo wa kumzuia, alimuacha afanye alichokitaka na sasa ni mwalimu wa sanaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,097FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles