33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MWONGOZO MPYA WA BARABARA VIJIJINI WAZINDULIWA

Na ESTHER MNYIKA -DAR ES SALAAM

SERIKALI imetangaza mwongozo mpya wa usanifu na ujenzi wa barabara zinazopitisha magari machache, hasa maeneo ya vijijini ambao utasaidia kupunguza gharama za ujenzi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa kitabu chenye mwongozo huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, alisema mwongozo huo unatoa maelekezo kwa wakandarasi wanaotengeneza barabara za vijijini.

Alisema utasaidia kupunguza gharama za ujenzi na usalama wa barabara tofauti na kipindi cha nyuma, ambako walikuwa wakitumia gharama kubwa.

“Kipindi cha nyuma, wizara yangu ilikuwa inatumia miongozo ya barabara kuu na za mikoa, hii ina gharama kubwa kutokana na kukosa mwongozo wa barabara zinazopitisha magari 300 kwa siku, kuepuka gharama hizi tukaanda mwongozo huu,” alisema Mhandisi Nyamhanga.

Aliwataka wahandisi na mafundi ujenzi watumie mwongozo huo katika utekelezaji wa majukumu yao ili kusaidia kazi na miradi mbalimbali ya barabara kuweza kufanyika kwa viwango vilivyo bora na gharama nafuu.

“Hakikisheni wahandisi na mafundi ujenzi mnafuata mwongozo huu ipasavyo kuanzia sasa, uwe dira kwenu katika kazi zenu za kila siku,” alisema Mhandisi Nyamhanga.

Alisema kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa, Serikali imegundua uhitaji mkubwa katika mtandao wa barabara ili kusaidia maendeleo ya kila mwananchi mijini na vijijini.

Mhandisi Nyamhanga alisema barabara za vijijini zilikuwa hazina miongozo, hivyo walikuwa wanatumia miongozo ya barabara hizo ambazo kwa siku zinapitisha magari 20,000 hadi 15,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles